Mapishi

Far za masiku tele mpendwa. ..? Na lil angel nae anaendeleaje? Busy siku hizi Hausikiki sana

Nzuri tu habibty angel wangu hajambo anaendelea vizuri....hahahaha busy na pirika za kulea

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
bibi mi napenda
Egg/meat chop:
Mahitaji


  • Nyama kilo moja

  • Mayai kumi

  • Kitunguu maji kimoja kikubwa

  • Kitunguu saumu kijiko cha chai 1

  • Tangawizi kijiko cha chai kimoja

  • Chumvi kiasi

  • Pilipilimanga kiasi

  • Mkate nusu

  • Kotmiri kiasi

  • Mafuta ya kukaangia

Jinsi ya kutayarisha
  1. Chemsha mayai 6
  2. Roweka mkate kwenye bakuli la maji ulowane ka dakika 5-10 ukishalainika ukamue maji
  3. Menya kitunguu na ukisugue kwenye bati ya kusugulia carrot yaani itatoka ka uji uji au kata lkn very finely.
  4. Nyama hakikisha kavu ikamue maji yote
  5. Weka vitunguu saumu,tangawizi,chumvi,pilipili manga,changanya na nyama.
  6. Weka ule mkate ulolowana,vile vitunguu ulivyosaga vikamue maji pia viwe vikavu na yai moja kisha changanya tena.Mwisho weka kotmiri
  7. Wacha mchanganyiko wake upumzike viungo vikolee like 1-2hrs weka kwenye fridge.
  8. Mayai yakishaiva yaache yapoe
  9. Chukua ule mchanganyiko wako fanya donge moja usawa wa mayai,tumia kiganja cha mkono na vidole kutengeneza kama chapati ienee mkononi.weka yai ulochemsha katikati kisha hakikisha yai lote linazibwa na hio nyama!Fanya hivo mpaka mayai yaishe.
  10. Weka mavuta yapate moto
  11. chukua mayai mawili yalobakia yapige kwenye bakuli au sahani,ichovye eggchop kwenye huo mchanganyiko wa mayai kisha ideep fry mpaka iive!
Eggchop tayari kwa kuliwa πŸ™‚
 
Nlikuwa wapi mie.
Well napenda sana dagaa kwa ugali dona,wali maini roast,chips yai na wali mchuzi mayai.
Nitaweka recipes kesho wapendwa nimechoka sana.
 
Nlikuwa wapi mie.
Well napenda sana dagaa kwa ugali dona,wali maini roast,chips yai na wali mchuzi mayai.
Nitaweka recipes kesho wapendwa nimechoka sana.

pole sana amu
ninasubiri kwa hamu hilo pishi
 
Last edited by a moderator:
pole sana amu
ninasubiri kwa hamu hilo pishi

Kupika dagaa
1.wachambue dagaa kea kuwatengenishe kichwa na viwiliwili vichwa natupa.
2.bandika sufuria au frying pan ikishapata moto weka dagaa wageuze geuze mpaka wawe brown kisha weka maji waoshe vizuri sana watoke michanga.

2.bandika sufuria jikoni wrka mafuta kiasi kwa kukaangia vitunguu maji, mafuta yakipata moto weka vitunguu maji kaanga vikiwa brown wrka nyanya zako zifunikie kidogo zichmke ila nyanya zisiive zitaiva na dagaa.Wekq vitunguu swaumu,dagaa kaanga kisha ufunikie na uwe unakaanga kaanga mpaka dagaa,nyanya na swaumu viiive.
Weka ile curry powder na nyanya pakti kama unayo acha mpaka nyanya pakti iive kisha weka karot hoho vikishaiva weka ndimu na chumvi vikichemka onja kama kila kitu kipo sawa kama pilipili wapenda tupia pilipili 1 kwa juu nzima kisha ipua tayari kea kuliwa.

Well ugali najua haukupi shida.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Mchuzi mayai nlishaweka humu.

chips kyepe he he ntakuwekea kesho pamoja na roast maini ya kulia ubwabwa.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…