Mapokezi ya Rais akitokea Marekani kwenye UNGA ni ufujaji wa kodi za walalahoi

Ukiona harakati za namna hii, ujue kuna jambo kiuongozi haliko sawa. Hivyo kuna makundi ya watu wanahangaika/wanalazimika kumtia moyo mama hata pale anapoharibu au ameshindwa kufikia matarajio ya Watanzania walio wengi
Hii tabia ya kishenzi ndio ilimponza Magufuli hadi akafa.
 
Watu wengi walioteuliwa na Marehemu Magufuli walikuwa ni watu wenye uelewa mdogo, exposure duni, wasiojiamini, wanafiki, wasio na weledi, na kwa kiasi kikubwa, kwa sababu ya kukosa sifa zinazostahili, waliegemea kwenye kumsifu ili kuendelea kuwepo kwenye nafasi zao. Watu hao mpaka sasa bado wapo Serikalini.

Hao ndio wanaofanya upuuzi kama huu wa kulifanya tendo la Rais kurudi nyumbani ni la ajabu.
 
Harakati za maendeleo zinajengwa na ushirikiano wa kimataifa big up Rais Samia umeitangaza Tanzania kidiplomasia
 
Karibu mama yetu kipenzi umeupigaa mwingi ng'ambo
Waswahili kwa akili Kama hizi nchi haitosogea kwa sababu mpk Sasa hivi sijaelewa mama kuupiga mwingi Ni kuongea kingereza uko UN au Kuna agenda nyingine muhimu za kitaifa amefanikisha uko UN?
 
Maajabu haya.

Unakuta aliyemwandalia hotuba, ndiye anayemwandalia mapokezi.
Let think
 
Gharama ya serikali? Unafahamu kuwa hizo gharama ni kodi wanazonyonywa watanzania?
Kodi inakusanywa ili itumike, hayo ndiyo moja ya matumizi yake, mengine ni kujenga barabara, zahanati, kulipa mishahara, kujenga mashule, kuhakikisha wewe unalindwa mipakani na hapo nyumbani kwako, ukisafiri (kama ni muajiriwa) kukuhakikishia utalala sehemu salama na nzuri na utakula, kumtunza Rais wa nchi na mengineyo..Ni utaratibu uliopo dunia nzima Mjomba!! Hata huko UN walikoenda hao akina Samia wamehudumiwa kwa kodi zilizotolewa na Raia wa nchi nyingine!! Au unataka hiyo Kodi Mwigulu aikalie pale wizarani hadi itage mayai?? TUMIA HELA UPATE HELA
 
Kwa hiyo hutaki tumpokee na kumpongeza Rais wetu au?

Ulitaka apokelewe baba yako au? Pumbavu,haters mtakufa kwa pressure bure..

Mda uliotumia kuandika upupu ungetumia kutafuta pesa usingekuja na malalamiko ya kipumbavu hapa.
Hakuna asietaka MH. RAIS apokelewe zifuatwe protocol za kawaida za kumpokea Rais lakini tusiweke sherehe zisizokua na tija zinatugharimu Kama Taifa.
 

Hizi ndo fikra za maCCM, majitu majinga kweli. Sasa anapokelewa kwamba kafanya nini la ajabu? Mkutano wa Umoja wa Mataifa ni sehemu ya nyororo ya dhahabu mikononi mwa waafrika.
 
Yaan nchi ngumu hii bas tu 🤣🤣🤣🤣
 
Rais hahusiki 100% na kesi zilizoko mahakamani......

Huyohuyo ndiye aliyewaambia POLISI WASIONEE RAIA....

Huyohuyo ndiye aliyesema KESI ZISIZO NA MAANA ZIFUTWE.....

Huyohuyo ndiye aliyemteua Dr.Eliezer Feleshi....muda UTAONGEA.....
Wanasisasa unawaelewa vizuri ama unawasikia tu?
 
Yaani ni ujinga mtupu....hawa waliotoa wazo hili hembu wajitafakari km wana akili timamu au ndio wizi wenyewe wa pesa za umma.....very stupid!
 
Bado wasomi wanasoma wapate ajira. Siwashangai.

Nitakapokuwa Rais . Watanifanyia hivi hivi kunisifu kwiiiiingi nina hekima, mzalendo namba 1.

Nisifuni sasa. Maana huu ujinga wa kupiga makofi nitawafukuza wengi sana
 
Tukimpokea atajisikia vizuri. Twendeni tukampokee tu. Ni njia moja ya kumtia moyo. Tulishasikia Urais siyo kazi nyepesi.
 
Ninakumbuka nimewahi kwenda JNIA kwa gharama zangu kwenye hafla ya kuipokea ndege.

Hata huku mtaaani wananchi wanahamasishana kwenda JNIA kumpokea rais. Kule hakuna gharama za Serikali wala chakula wala nauli, na hata mtoa mada mwenyewe umeona tangazo lako halina maelezo ya gharama zaidi ya hamasa.

Watu wanaenda huko kwa mapenzi na gharama zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…