Mshombsy
JF-Expert Member
- Mar 15, 2013
- 372
- 180
Rasimu ya katiba ibara ya 12 sera ya mambo ya nje inaonyesha kwamba nchi yetu inayo majukumu kwenye jumuiya ya kimataifa. Sera hiyo inaongelea kukuza ushirikiano wa kikanda na kimataifa kwenye nyanja za kiuchumi, haki za binadamu, uhuru wa watu, kupambana na makosa ya jinai ya kimataifa na pia inatamka kuheshimu mikataba ya kimataifa.
Kati ya mikataba ambayo tunalazimika kuiheshimu ni ile ya kupambana na makosa ya jinai ya kimataifa kama biashara ya ngono kwa watoto wadogo. Katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi itabidi kuheshimu mikataba ya kupambana na fedha haramu. Tutaheshimu mikataba ya kupambana na uhalifu wa haki za binadamu kama kweli sera ya mambo ya nje ina lengo la kukuza uzingatiaji wa haki za binadamu.
Sasa katika kumpana na makosa hayo lazima nchi yetu itaingia mikataba (bilateral treaties) ya kubadilishana wahalifu (extradition) kwa nchi ambazo hatujasaini. Kuna nchi ambazo tayari tuna mikataba ya namna hii mfano Marekani mwaka 1931 uliyosainiwa upya mwaka 1965 baada ya kupata uhuru, Kuna uholanzi mwaka 1968 na nchi nyingine tuna makubaliano tu kama India mwaka 1966 na Thailand mwaka huu. Mikataba hii inaongozwa na sheria namba 15 ya mwaka 1965. Kuna mtu atafanya uhalifu hapa nchini na kukimbilia nje tutaiomba nchi aliokimbilia arejeshwe nchini kujibu mashtaka yanayomkabili. Hivyo mtu akifanya uhalifu nchi nyingine na kukimbilia hapa tumrejeshe baada ya taratibu zote kufuatwa.
Mbali na mikataba ya ushirikiano na mataifa mengine kupambana na uhalifu, tuna sheria zetu zinazotamka hata mtu akiwa nje ya nchi anaweza kuhesabiwa ametenda kosa hilo hapa nchini. Mfano ni sheria ya kupambana na ugaidi namba 21 ya mwaka 2002. Hivyo hata wahalifu wa kosa hili tutataka waletwe nchini kujibu mashtaka.
Historia inatufundisha kwamba binadamu waovu wako wengi na tunaandika katiba mpya kwasababu raia na viongozi waovu wametufikisha hapa tulipo hivyo lazima tuwe na ushirikiano na mataifa mengine katika kupambana na uhalifu. Tusiandike katiba itakayotubana kutimiza wajibu wetu kama taifa kwenye jumuiya ya kimataifa na kushindwa kupambana na uhalifu utakaotokea hapa nchini.
Nimeanza na maelezo ili niweze kuonyesha mapungufu rasimu ya katiba ibara ya 39(3). Ibara inasema Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake. Kati ya njia wanasheria wanazotumia kufikia uhamuzi wa kesi mojawapo ni kufuata maandishi (textual) kama yalivyotumika kuiandika sheria husika ikiwa maneno yake hayana utata. Ibara ya 39(3) haina utata wa maneno kwa maana kama mtu anatuhuma nje ya nchi ni ridhaa yake kwenda kukabili mashtaka na kama hataki basi.
Maneno ridhaa yake yaondolewe na uwekwe utaratibu wa kapitia mahakamani kama sheria inayosimamia ubadilishanaji wahalifu inavyosema. Hata ukisoma mkataba wa ubadilishanaji wahalifu kati yetu na Marekani umeweka utaratibu mzuri wa kufuata wa kupitia mahakamani, kuonyesha kiwango fulani cha ushaidi. Vilevile hairuhusu wahalifu wa kisiasa kurudishwa makwao. Inawezakana hapo nyuma utaratibu ulikuwa haufuatwi kwasababu hakukuwa na kifungu kwenye katiba kinachotoa utaratibu wa jambo hili. Vilevile ibara hiyo isiusishe raia tu bali na raia wa kigeni wanaoishi nchini hata kama hawaishi kihalali ili kulinda haki zao kibinadamu. Hatutaki serikali ya nje iseme raia wake arudi kujibu mashtaka na sisi tumkabidhi hata kama aendako hatapata haki yake ya kusikilizwa.
Mimi siyo mtaalam wa sheria lakini kwa uelewa wangu mdogo hakuna sheria yoyote au mkataba wowote wa kiushirikiano na mataifa ya nje utakuwa na nguvu kuliko katiba ya nchi. Tunapoiandika katiba mpya tujue tayari zipo sheria na mikataba ambayo tumeisaini na tutalazimika kuiheshimu. Ibara hii ikipita jinsi ilivyo italeta msuguano wa kidiplomasia mbeleni na sisi tutashindwa kupamba na uhalifu kama uhujumu uchumi na ugaidi.
Wote tunakumbuka watu walivyotaka Gavana wa benki kuu Daudi Balali arudishwe toka Marekani aje kujibu tuhuma za EPA. Serikali ilisema ina mkono mrefu kama ikimuitaji lakini kwa ibara hii mkono wake utakuwa umekatwa.
Katika mikataba ya kubadilishana wahalifu kila upande lazima uwe na uhakika kwamba ukiomba mtuhumiwa arudishwe kujibu mashtaka atarejeshwa. Sisi tutakuwa tumejifunga tena wakati ambao tunafatilia mabilioni ya uswiss. Hakuna taifa lolote litakalokubali kuingia mkataba wa kubadilisha wahalifu na sisi kwasababu wanajua raia wa Tanzania akitenda kosa akakimbilia Tanzania ni ridhaa yake si mahakama kuamua hata kama ushaidi upo.
Inawezekana ibara hiyo imewekwa watu wakiwa na mawazo ya Marekani kupeleka watuhumiwa wa ugaidi kwa siri (rendition) bila kuangalia njia mbadala itakayotufanya na sisi kuletewa watuhumiwa wanaokimbilia nje baada ya kufanya uhalifu hapa nchini. Kuna milipuko ya mabomu Arusha, serikali ilitoa milioni 100 kwa atakayetoa taharifa kwa wahusika: hivi tukiambiwa wamekimbilia nje ya nchi tutaiomba nchi ambayo utaratibu wa kukabidhi mtuhumiwa imeiachia mahakama wakati sisi kifungu kiko wazi ridhaa ya mtuhumiwa? Nchi nyingi utaratibu wa kukabidhi wahalifu kwa taifa jingine unahusi hata wasio raia, mfano Uganda imekataa kuwatoa viongozi wa waasi wa M23.
Hivi ikiwa mtanzania ametenda kosa la jinai akiwa nje ya nchi dhidi ya mtanzania mwenzake na akakimbilia Tanzania kwa sababu anajua itakuwa ridhaa yake hata akigundulika, huyu atashughulikiwa vipi ikiwa nchi alikotendea kosa ina muhitaji kujibu mashtaka? Mfano, Mtanzania Peter Kupaza yuko jela Marekani kwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumuua binamu yake Ovino Kupaza kwa kumkatakata na kutupa vipande vya mwili wake (Wisconsi v. Peter T. Kupaza). Vielelezo vya ushaidi vilikuwa vingi dhidi yake kuonyesha ametenda kosa hilo la jinai. Sasa kwa ibara hii kama serikali ya Marekani ingetaka arudi Jimbo la Wisconsin kujibu tuhuma ingekuwa vipi maana ni ridhaa yake? Na mtanzania mhanga wa unyama huo nje ya nchi haki yake anaipata wapi?
Tukumbuke ya kwamba wahalifu wote uwa na mlango wa kutokea (exit plan) mambo yakienda kombo na mara nyingi wanajua nchi zenye udhaifu wa sheria za kuwakabidhi watuhumiwa kwa kuangalia kama wana mikataba na nchi walikotendea kosa mfano Alex Masawe nasikia yuko Dubai na ana uraia tayari. Wengine watakimbilia nchi nyingine ambazo wanaona hata wakifungwa jela za huko sio kama za nchi zao. Mnakumbuka Generali Ntaganda muasi wa Kongo alijikabidhi mwenyewe kwenye ubalozi wa Marekani Kigali na wao wakamkabidhi mahakama ya kimataifa ambako anajua kabisa mazingira ya jela Uholanzi si kama Rwanda au Kongo.