Mapungufu ya Dini za Wakoloni

DR.MBWEMBWE

Member
Joined
Nov 27, 2012
Posts
19
Reaction score
20
KAMA ULIKALILI TU MAANDIKO KAA PEMBENI HAUKUHUSU

Kama mafundisho ya Dini yanatuambia kuwa Mungu ananijua kabla hata sijazaliwa, maana yake anajua kila kitu ninachofanya na hadi nitakacho fanya baadae (kwa future)

(A) Maana yake mimi siwezi kwenda kinyume na anachokijua Mungu, sasa hii kauli ya kusema nimetenda kinyume na mapenzi au mpango wake inatokea wapi? Kwani kabla sijatenda je alijua kama nitatenda kinyume na mapenzi au mipango yake? (NDIYO/HAPANA) k

(B) Kama alijua kabla sijazaliwa kuwa nitatenda kinyume na mapenzi yake sasa kwanini kama nikitenda kinyume na mapenzi au mipango yake anachukia? Na kama hakujua kama nitatenda kinyume basi je kwanini anaitwa Mungu mjua vyote?

Swali jingine
(C) Je, kuna mtu anaweza kubadilisha mapenzi au mipango ya Mungu? (NDIYO/HAPANA)

kama ni jibu ni NDIYO kipengele C litazaa swali hili

(D) Je, huyo Mungu ambaye anakujua kabla hujazaliwa je alijua before kuwa utakuja kubadili mapenzi au mipango yake? (NDIYO/HAPANA)

Kama jibu ni HAPANA kipengele C basi huyo Mungu hastahili kupewa sifa ya mjua vyote.(Omniscient)

Kama jibu ni NDIYO kipengele D. Maana yake ni kwamba bado hujabadili alichokuwa anajua. Sasa kama huwezi je kwanini unapoteza muda kumuomba akusaidie kutatua matatizo yako? Maana hata ukiomba na kulia kwa machozi ya damu hawezi kubadili mpango wake juu yako.

Kama jibu ni HAPANA kipengele D. Maanake huyo Mungu hakujua kuwa utabadili mipango yake.

Huyu Mungu wa kwenye Hivi Vitabu hii sifa ya kuwa yeye ni mjua yote, hapana sio mjua yote, hata maandiko ya hivyo vitabu yanadhihirisha kuwa yeye si mjua yote.

Mjua yote hawezi kuwa na hasira maana hasira inakuja pale unapopata au kufanyiwa kitu ambacho hukutarajia, hukujua.

Sasa cha kushangaza hadithi za hivyo vitabu vinadhihirisha kuwa huyo Mungu kuna wakati alipatwa na hasira, ghadhabu, hata kukata tamaa.

Rejea
Kutoka 32:10
Mwanzo 6:6
Ukihitaji rejea nyingine nifahamishe.

AMKENI MJITAMBUE
IMEANDALIWA NA FRANK A. CHALE
 
Sasa unataka nani aabudiwe? Uwezo wa Mungu hauchunguziki kwa jinsi ya mwili yaani akili za mwili. Mambo ya rohoni hujulikana roho tu
 
Omniscience is incomprehensible.

Ujuzi wa vyote ni kitu kisichowezekana, bora hata ujuzi wake ungekuwa wa maarifa ya kidunia tu, ila upo temporal(anajua yajayo) ni hadithi kwa kweli.
 
Tushapigwa mpwa . Fungu la 10 nao utapeli tu
 
Ni uhuru wa binadamu pia kukashifu kila anachokiona hakina mantiki.

Yahweh anasema aliumba binadamu wote. Hivyo binadamu wote wanapaswa kumuabudu.

Lakini dini ya ukristo ilifika Tanzania maelfu ya miaka baada ya kuanza kwake. Na sio kwa nia nzuri.

Pia kama dini yake ndo ya kweli mbona anaruhusu watu kuabudu miungu mingine mf Allah?

Ni maswali yanayopaswa kujibiwa.
 
Pre-determinism ni mojawapo ya mambo pasua kichwa kabisa kuyaelewa na kuyapatia majibu kwa kutumia mantiki ya kawaida.

Mhubiri mmoja mashuhuri sana na msomi kweli kweli wa Thiolojia aliwahi kuulizwa kwamba itakuwaje kama Yesu Akirudi halafu akute watu ambao hawajawahi kusikia Injili yake. Je watu hao ambao hawajawahi kusikia habari zake watakwenda motoni au mbinguni?

Alisema kwamba watu hao watakwenda motoni maana kwenda mbinguni ni lazima kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi. Lakini pia akapendekeza kwamba baadhi yao wanaweza kwenda mbinguni kwa sababu Mungu Anajua ni wapi kati yao wangempokea Yesu hata kama ingetokea wakahubiriwa; na kwamba hili Mungu Analijua na Alilijua hata kabla hao watu hawajazaliwa. Yaani Mungu Ali/najua watu ambao watakwenda mbinguni na ambao watakwenda motoni hata kabla watu hao hawajazaliwa!

Swali likaja kwamba: Je inawezekana mtu aliyekuwa predetermined kwenda motoni akapambana mpaka kubadilisha fate yake ya kwenda motoni na hatimaye kuishia mbinguni?

Niishie hapa maana maana huwa nikifikiria haya mambo kichwa huwa kinaishia kupata moto. Na mimi huwa nakiri kwamba kuna mambo kumhusu Mungu Ambayo sitakaa niyajue kamwe! Na kusema kweli nisingependa kumwabudu Mungu Ambaye najua kila kitu kumhusu 🙏🏿
 
Sasa kwanini mungu aghadhibike kwa kile ambacho anakijua?

Ni kwamba mungu ni mhusika wa kufikirika. Ametungwa na binadamu.

Na akapewa hizo sifa za kiungu, ili watu wamtumie kujibu maswali yasiyo na majibu.

Lakini kimantiki, miungu ni vitu vya kipuuzi mno.

Ni bora kukubali kuna maswali hayana majibu, kuliko kuamini yanajibiwa na kiumbe kisicho na mantiki.
 
(D) Je, huyo Mungu ambaye anakujua kabla hujazaliwa je alijua before kuwa utakuja kubadili mapenzi au mipango yake? (NDIYO/HAPANA)
Kama ndiyo kwanini hakukasirika muda huohuo?
 
Mhubiri mmoja mashuhuri sana na msomi kweli kweli wa Thiolojia aliwahi kuulizwa kwamba itakuwaje kama Yesu Akirudi halafu akute watu ambao hawajawahi kusikia Injili yake. Je watu hao ambao hawajawahi kusikia habari zake watakwenda motoni au mbinguni?
Kama wale Bushmen wa The Gods must be crazy
 
Ni muhimu pia kuzingatia kwamba dini zilikuwa zinaenea ulimwenguni kote kupitia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na biashara, utamaduni, na mawasiliano ya kibinadamu. Kwa hiyo, mchakato wa kueneza dini ulikuwa ni wa kimataifa na wa kubadilishana.
Mkicheka chekeni kwa uangalifu kuna wachungaji humu

 
Kuelewa unachouliza unatakiwa ufanye summary ya mambo mawili

-mwenyez mungu anajua Kila kitu
-Binadamu ana free will.

Ukiweza kufanya hizo statment mbili ku Co-exist basi utakua umeshapata jibu la maswali yote ya juu.

Na ili uweze kuzifanya hizo statement ku Co-exist pamoja chukulia mfano wa computer ama game.

Developer anatengeneza Program ya computer anaweka maelfu ya features, Developer anajua features zote, wewe unatumia hio program una free will kuchagua feature yoyote ile ila hakuna feature hata moja ambayo utachagua ambayo developer haijui.

Mwenyez Mungu alitengeneza Dunia way before hata Binadamu wa kwanza hajakuja, Kila kitu kimeandikwa, wewe una free will kufuata ambavyo mwenyez Mungu ameweka, ila ni will yako inayoamua kufuata vitu vizuri vilivyowekwa na Mwenyez Mungu ama kufuata vitu vibaya.
 
Ko
Ko unataka umwabudu Mungu usiyemjua. Kwani usipoabudu unapungukiwa nini? Au unaogopa moto
 
Hapo katika hiyo Freewill, linazaliwa swali jingine tata, kama amenipa uhuru wa Kuchagua, vipi je kabla sijachagua Mungu anajua nitachagua nini?
 
Kujua kila kitu maana yake ni kujua kila kitu. Yaani kila kitu kuhusu maisha yako labda kuna siku utagombana na mtu flani, utaachwa na mkeo nk

Sasa maana yake ni kwamba hadi machaguzi yako anayajua. Hivyo hamna 'chaguzi huru'
 
Hapo katika hiyo Freewill, linazaliwa swali jingine tata, kama amenipa uhuru wa Kuchagua, vipi je kabla sijachagua Mungu anajua nitachagua nini?
Ndio jibu hapo nimekupa juu, Mwenyez Mungu anajua outcome ya ulichochagua, mwenye will ya kuchagua ni wewe, you have trilions of choice na outcome za Choice zote Mwenyez Mungu anazijua.
 
Hapana sio kwamba ni magumu, bali yanajichanganya sema kwasababu tumekuwa brainwashed tangu utotoni, na tumekalilishwa kuwa maandiko ya mungu huwezi kuyaelewa kwa akili za kibinadamu wa huwezi kuyakosoa, hii ndio inawafanya watu wawe waoga na kushindwa kugundua mapungufu ya hizi Dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…