Mndengereko
JF-Expert Member
- Mar 24, 2011
- 7,296
- 3,398
UTAWALA (BORA)
Uwepo wa Uongozi na serikali mbalimbali una lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi wanaowaongoza na njia mojawapo ambayo ni kiungo muhimu cha kufikisha maendeleo hayo kwa wanachi hao ni utawala, hivyo utawala ambao ni bora ukizingatiwa ni wazi maendeleo na matokeo chanya yatapatikana
Kwa mujibu wa umoja wa mataifa ,utawala bora unatakiwa kuwa na sifa zifuatao
1-uwe ni utawala wa sharia (kila mtu awajibike kulingana na sharia zilizopo)
2- uwazi
3-uwajibikaji
4-ubora na ufanisi (effectiveness and effiency)
5-usawa na ujumuishwaji wa kila mmoja (equity and inclusiveness)
6-ushiriki wa kila mmoja/makundi muhimu/maalum katika maamuzi
7-mrejesho kwa wanachi /wadau juu ya mambo mbalimbali (responsiveness)
Changamoto mbalimbali za kiutawala tuliokuwa nazo katika jamii yetu zinaweza kutatuliwa kwa kufanyika na kuacha kufanya yafuatayo;
a/polisi kuacha kuita vyombo vya habari na kuanza kuwataja wahalifu ambao wamewakamata ,tena huwaonyesha kwa majina yao pamoja na utambulisho wa picha(zao) kwani kufanya hivyo ni kosa kwa utawala wa kisheria, ambapo kila mmoja ni msafi mpaka atapokutwa na hatia,hivyo kama kuna ulazima wa kutoa taarifa kwa jamii basi maafande wa polisi wa mikoa ni bora wakaficha utambulisho wa majina na sura wa wahalifu/watuhumiwa hao, mpaka mahakama itakapotoa hukumu,mtuhumiwa aliyetangazwa ikitokea mahakamani ameshinda tofauti na matarjio ya idara ya polisi/serikali anaweza kuishtaki seriklai kwa kosa la kumdhalilisha(defamation)
b/ili kulipa bunge nguvu na kuliongezea uwezo wa kuiwajibisha na kuisimamia serikali,kwenye dhana ya mgawanyo wa madaraka ni vyema mawaziri wasiwe sehemu ya wabunge kama ilivyo hivi sasa ,kwani kufanya hivyo ni kulipunguzia bunge nguvu ya kuihoji serikali na hata wabunge hao ambao ni mawaziri wanapata wakati mgumu kutumikia nafasi mbili kwa wakati mmoja na hivyo upunguza ufanisi wa kazi.
c/mahakama ni chombo muhimu sana katika utawala bora na utawala wa sheria,changamoto nyingi za kiutawala zinaweza kurekebishwa kwa kupitia chombo cha mahakama na uhuru wake kamili,kwa Tanzania kwa jicho la kawaida tu linaonesha kuna udhaifu wa utendaji kazi wa mahakama hasa kwa rais wa nchi kuwa mteule wa jaji mkuu na majaji wa mahakama kuu,ili majaji hawa wawe huru kufanya majukumu yao ni bora wakawa wanateuliwa na chombo kingine mfano tume ya utumish wa mahakama (judicial service commission)
d/kuongeza uhuru zaidi wa ufanyaji kazi wa idara ya mahakama ni vyema pia mahakama ikawa na bajeti yake katika ufanyaj kazi,tofauti na sasa ambapo hutegema bajeti ya serikali ,hivyo inawezekana wakawa wanalazimika kutekeleza matakwa ya serikali ili waweze kupata mgao wa kujiendesha
e/ kumekuwepo na matukio ya kujirudia rudia na yanyofanana, juu ya watu kupotea na kisha kuambiwa walikamatwa na watu wasiojulikana na wengine hata hufa, matukio haya yanaweza kupungua iwapo tume ya haki za binaadamu ambayo imetajwa katika katiba itakuwa na nguvu ya kutosha katika ufanyaji kazi wake, ambayo mojwapo ya jukumu lake ni kuhamasisha nchi juu ya uhifadhi wa haki za binaadamu, ambapo pia tume hii imeruhsiwa kuchunguza matukio kadhaa,kupokea malalamiko na hata kufungua shauri mahakamani kupinga matukio kadhaa ya ukikuwaji wa haki za binaadamu ,pamoj a na kuwa tume hii inatambulwa kikatiba na hata kutajwa katika ibara ya 129,kiuhalisia tume hii haina nguvu kwa kuwa mwenyekiti ,makamu mwenyekiti wake wote ni wateule wa raisi wa nchi pamoja na makamishna wake, hivyo ili kuleta tija ni bora mwenyekiti,na makamishana wa tume hii wasiwe zao la mamlaka ya rais na badala yake watokane na kamati ya uteuzi ambayo ina wajumbe,spika wa tanzania, spika wa baraza la wawakilishi,naibu mwanasheria mkuu wa serikali,na jaji mkuu
f/ tume hii ya haki za binaadamu ina changamoto nyingine kubwa ambayo ni kuwa haina uwezo wa kufanya maamuzi ,zaidi ni kuandika ripoti na kutoa mapendezo ,hivyo ni vyema ikapewa nguvu ya kisheria ya kuwa mapendekezo yake yote ni lazima yatekelezwa na serikali pindi yawasilishwapo
g/kuongeza ushiriki wa wananchi katika maamuzi,nchi yetu ina mfumo mzuri sana wa kutaka wananchi washiriki katika maamuzi hasa ya serikali za mtaa,lakini bahati mbaya wananchi wengi hawashiriki kwa kutojua na uzembe wa viongozi ,mfano kwa mujibu wa sheria ya serikali za mtaa ya 1982 inataka kila baada ya mwezi kufanyike mkutano mkuu wa kitongoji na kila baada ya miezi mitatu ufanyike mkutano mkuu wa kijiji ,lakini maeneo mengi mikutano hii haifanyiki na wananchi wanashindwa kupata fursa rasmi ya kuzipima serikaliza zao za mitaa, na kufanya maamuzi au kutoa ushauri –nini kifanyike viongozi wa serikali za mitaa ambao hawafanyi mikutano hii na hawashirikishi wananchi katika maaumuzi ni vyema wakachukuliwa htaua za kuondolewa madarakani hili litasaidia mikutano kuwa inafanyika na wananchi kushiriki katika kujenga nchi yao na changamoto ndogondogo za kazi za kijiji,kata kumalizwa kwa haraka tofauti na sasa hata changamoto ndogo inasubiri ujio wa kiongozi mkubwa wa ngazi ya kitaifa
h/kubadilisha ufanyaji kazi wa idara ya polisi hasa katika vituovya polisi ,sheria inaelekeza mtuhumiwa akamatwapo ndani ya masaa 48 afikishwe mahakamani lakini kwa uzembe wakuu wa vituo vya polisi wamekuwa wakikaa na watuhumiwa hawa zaidi ya masaa hayo katika vituo vyao bila ya kuwapeleka mahakamani, na hivyo kuchochea mazingira ya rushwa,ili kukomesha hili serikali inaweza ikaweka utaratibu wa kuwataka wakuu wa vituo vya polisi wa wapeleke mahakamani wahalifu ndani ya masaa hayo vinginevyo wawachie na kama kutakuwa na unalazima wa kukaa nao zaidi ya masaa hayo basi kibali cha mkurugenzi wa makosa ya jinai(DPP) kitolewe na wakuu wa vituo watakaokiuka utaratibu huu wa chukuliwe hatua kwa mujibu wa utaratibu utakaokuwa umewekwa
i/kero ya traffic barabarani – matrafic wamewekwa wengi barabarani kwa lengo la kupunguza ajali na kutoa msaada wa haraka wa kiusalama barabarani, lakini matokeo yake matrafic hawa wengi wao wamekuwa ni watu wa kuchukua rushwa tena mchana kweupe kabisa ,kwa magari madogo na hata kwa mabasi ya umma ,na hata kufikia hatua wenye magari kuona ni kero na mara nyingi huandaa kama waitavyo
bakshishi ya sh 2,000-10,000 na kumpa traffic ili asikague gari na hata kama ni gari la abiria huachwa hata kama lina kosa mfano la kujaza abiria kupita kiasi n.k ,nini kifanyike matrafic wapunguzwe barabarani na badala yake mifumo ya kidigitali ichukue nafasi mfano zifungwe kamera kwa wingi barabarani zitakazokuwa zinakagua magari yafanyayo makosa,pili badala ya matrafiki kufanya kazi ya uongo ya kukagua gari kwa muda mchanche wayasimamishapo ni bora kukawa na idara maalum ya serikali itakayokuwa inatoa cheti pindi gari ikaguliwapo kifundi na kuonekana ni nzima na kukidhi vigezo ,hivyo traffic asimamishapo badala ya kumwambia derva akanyage breki ili akague kuona kama breki ya gari ni nzima anaonyewshwa cheti tu. Kinachotolewa na serikali au mawakala wa serikali walioidhinishwa na kinachothibitisha gari imefanyiwa matengenezo (service)j/wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuwa wenyeviti wa kamati za maadili ambapo kamati hizi huwa na nguvu ya kuwawajibisha mahakimu waliopo katika maeneo hayo husika,hii inaweza kupelekea mahakimu hawa wakawa wanafanya kazi kwa wasiwasi kwa kuogopa kuwajibishwa hivyo ni bora jukumu hili la kamati za maadili likafanywa na tume ya utumishi wa mahakama (judicial service commission)
i/kuweka ukomo wa muda kwa viongozi wa viti maalum kwani kwa sasa kuna baadhi ya viongozi wamejimilikisha uongozi huo,mfano madiwani na wabunge wa viti maalum,lengo la kuanzishwa kwa mfumo huu ni kuwajenggea nguvu na uwezo wanawake wa kushindana na wanaume katika maeneo ya uchaguzi mfano katika majimbo na kata,hivyo ni vyema ikawekwa ukomo kwa kiongozi wa viti maalum kuongoza mfano ikawa ni awamu 1 au 2 kwa maana kuwa atakuwa ashapata uzoefu wa uongozi kupambana rasmi katika aitha jimboa au kata na pia kutatoa fursa kwa viongozi wengine wanawake kuibuka
j/mwisho kwa sasa kupunguza nguvu ya viongozi wa vyama vya siasa kuingilia moja kwa moja serikali badala ya kuishauri tena katika vikao/mikutano ya vyama vyao rasmi,kumekuwa na tabia ya muda mrefu ambayo inaendelea mpaka sasa ya kuwa kamati za siasa (kata,wilaya,mkoa) hasa za chama tawala kutembelea miradi mbalimbali ya serikali na kutoa maagizo kwa viongozi wa serikali na bahati mbaya kuna baadhi ya maagizo hukiuka miongozo ya uendeshaji wa serikali,mfano wa hivi karibu ni katibu wa itikadi wa uenezi was C.C.M aliagiza kusimamishawa kazi kwa mrajisi msaidizi wa idara ya ushirikia mkoani tabora kwa kuwa kwenye mikutano yake aliyokuwa anapita mrajisi huyo alikuwa akilalamikiwa na wakati yaeye sio mamalaka ya nidhamu ya mrajisi huyo
Mwisho kwa kumalizia changamoto zote zinaweza kutatuliwa kwa Kuzingatia utawala wa sheria na uongozi bora
Mndengereko
Upvote
1