Mapya yazidi kuibuka uchaguzi SAUT

oneblood

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2011
Posts
244
Reaction score
51
wakuu, Mambo sasa si shwari tena chuoni SAUT,mgombea wa kiti cha urais wa chuo aliyeshindwa bwana Peter Bega,amekata rufaa kupinga kutangazwa mshindi bwana Dovakamwene Mcheshi,aliyeibuka mshindi kwenye uchaguzi wa nafasi ya urais chuoni hapo,uchaguzi huo uliofanyika tarehe 12/4/2013 chuoni hapo,katika madai yake ya msingi bwana Bega anayakatia rufa mambo yafuatayo,

1.Mchakato mzima kugubikwa na uchama,

2.Tume ya uchaguzi kuundwa na asilimia kubwa na wanachama wa CHADEMA

3.Anadai kuchakachuliwa matokeo

4. Anadai Kwenye chumba cha kuhesabia kura ,baadhi ya mawakala kuonyesha alama ya vidole viwili mala tu baada ya kuhesabiwa na kujumlisha matokeo

5. Kutumia mitandao ya kijamii (JF na facebook page ya CHADEMA SAUT)kumchafua na kumuhusisha na CCM hali iliyopelekea kura zake kupungua

7. Kuwashawishi watu wasimchague kwa kuwa ana SUPLEMENTALLY 2,

8. Kutuma sms za kumchafua

Kwa upande mwingine wanaCHADEMA SAUT wamemshukia vikali mwenyekiti wa BAVICHA bwana John Heche wakimlaumu kwa kutoa kauli ya kejeli kwa viongozi na wanaCHADEMA SAUT kwa kuwambia hawajafanya kazi yoyote ya maana kwenye uchaguzi huo kwa maana kwamba kama wangekuwa wamefanya kazi ipasavyo mwanachama wao alieshinda uchaguzi huo asingeshinda kwa tofauti ya kura 188 tu.

Akiongea mmoja wa wanachama alisema"me namshangaa bwana Heche yupo makao makuu na haelewi ni kwa jinsi gani uchaguzi huu ulikuwa mgumu,sababu CCM mkoa walikuwa wamemwaga fedha nyingi kuhakisha mgombea wetu anashindwa na wao ashinde,nashangaa leo anaibuka kiongozi mkubwa wa BAVICHA na kuanza kubwabwaja maneno ya kuudhi na kukatisha tamaa wakati hawakutoa msaada wa aina yoyote kwenye tawi ili kupambana na CCM na taarifa walikuwa nao za kila kilichokuwa kinaendelea.

"Mtakumbuka awali niliwadokeza wana JF kuwa uchaguzi huo sasa umechukua sura ya u-CCM na UCHADEMA kutokana na wagombea wote wawili kuwa wanachama wa vyama hivyo, na mpaka sasa kuna zinasema kuna mashinikizo kutoka CCM mkoa na baadhi ya wahadhili wa chuo hicho wakimtaka bwana Bega akate rufaa na huku ikidaiwa hata mwanasheria alia aliemwandikia rufaa hiyo fedha amepewa na CCM mkoa wa Mwanza.
 
Si vyema chaguzi vyuo vikuu zikawa za u-ccm na u-chadema, lakini kwa sasa hilo haliepukiki.Uccm na Uchadema vimetawala hata michezoni, nilishuhudia pale mwanza kirumba Yanga ccm, simba Chadema.so sishangai
 
Aache u-mbulula!!!! Kilichompeleka chuo ni masomo au kesi!!??

Hao mawakala si aliwachagua mwenyewe? Iweje analalamikia uchaguzi kugubikwa na u-ccm nz u-chadema wakati huohuo anatumia njia hiyohiyo kukata rufaa!!??
 
Kimsingi siasa vyuoni haiwezi kuepukwa kutokana na vyuo kuwa ndo 'think tank'ya nchi yoyote kwa kulitambua hilo vyama vya siasa vimekuwa vikijipenyeza vyuoni ili kuchota tank hizo bt imeonekana sikuhizi kufanya siasa vyuoni ni haramu kutokana na kuwa wasomi wengi hawaiungi mkono CCM na wanaviunga mkono vyama vya upinzani hasa CDM that why utasikia vijana vyuoni acheni siasa bt zamani walikuwa wakihamasisha wanachuo kujiunga na CCM,Sham to CCM, kunya anye kuku,akinya bata kaharisha.
 
Kazi nzuri mmefanya wabunge watarajiwa
 
Someni ndugu zangu acheni siasa kivile. Kama Rais kapataikana sasa shida inatoka wapi na wakati hapo chuoni nyie ni wapitaji tu?
 
CHADEMA ni wala rushwa na mafisadi ambao hawajapata nafasi bado. Ninachomshukuru Mungu ni kwamba haitakuja kutokea wakaingia ikulu.

Madai ya ndugu Peter Bega ni ya msingi.
 
CHADEMA ni wala rushwa na mafisadi ambao hawajapata nafasi bado. Ninachomshukuru Mungu ni kwamba haitakuja kutokea wakaingia ikulu.

Madai ya ndugu Peter Bega ni ya msingi.

Ukinyamaza haufi
 
Asanteni Moderators kwa kuniwekea vizuri uzi huu.
 
CHADEMA ni wala rushwa na
mafisadi ambao hawajapata nafasi bado. Ninachomshukuru Mungu ni kwamba
haitakuja kutokea wakaingia ikulu.

Madai ya ndugu Peter Bega ni ya msingi.

Sumu wewe nu mbulula kweli, hata kwenye ufikiri wako wa kipumbavu unamshirikisha Mungu. Acha kujiongezea laana juu ya laana
 
CHADEMA ni wala rushwa na mafisadi ambao hawajapata nafasi bado. Ninachomshukuru Mungu ni kwamba haitakuja kutokea wakaingia ikulu.

Madai ya ndugu Peter Bega ni ya msingi.


kinachonichekesha na kunivunja mbavu zangu ni kwamba sikuhizi hata nyie Magamba mnalalamika kama hamna serikali na vyama vya upinzani,shame.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…