Mjasiri na Mali
JF-Expert Member
- Jun 24, 2017
- 5,366
- 14,167
Mkuu napenda sana avatar yakoNina Amini Mungu yupo.
Ishara na Matendo yake nayaamini ingawa ni ngumu kumwelezea mtu akaelewa.
Kila kitu hutokea kwa SABABU...
1. Inawezekana mafanikio yako yakawa si yako mwenyewe na Mungu akawa hayupo. Kuna wazazi, walimu, mentors, wateja etc watakuwa wamekusaidia kupata mafanikio.Eti ooh haya mafanikio yangu juhudi zangu mwenyewe. Hakuna kitu kama Mungu... Nimesoma nakujituma. Kama Mungu yupo na ajionyeshe Sasa... Mara ukifa unamkuta huyu hapo ameketi kwenye kiti Cha enzi.....
Vipi kuhusu upande wa pili , shetwani yupo??1. Inawezekana mafanikio yako yakawa si yako mwenyewe na Mungu akawa hayupo. Kuna wazazi, walimu, mentors, wateja etc watakuwa wamekusaidia kupata mafanikio.
2. Mimi siamini Mungu. Nikikutana naye baada ya kufa, nitamshitaki kwake yeye mwenyewe, kwa nini alijificha sana nisimjue licha ya mijadala yote niliyoanzisha JF kujadili kwa maswali mapana na marefu nimjue, alinikosesha neema ya kumjua?
Nitamuomba atoe posts zangu zote za JF aone nilivyotafuta kumjua, nitamuuliza kwa nini hakunipa neema ya kumjua hata baada ya posts zote hizi? Nitamwambia kama sikumjua, hilo ni kosa lake yeye na si langu mimi, kwa sababu nilimtafuta sana na yeye akajificha sana nisimjue.
Kama anafuata haki itabidi aniachie tu.
Lakini hawezi kuniachia.
Kwa sababu hayupo.
Kama unabisha, thibitisha yupo.
Shetwani kama anavyoelezewa katika vitabu ni zao la Mungu, kwa hivyo, kama Mungu hayupo, na shetwani naye hayupo.Vipi kuhusu upande wa pili , shetwani yupo??
Mkuu napenda sana avatar yako
Imanininaweza kuwa yavjweli au uongo.Mungu huambatana na imani. Ili umjue lazima uwe na imani juu ya uwepo wake. Vinginevyo hata pale usikiapo habari zake hutaziamini.
Uko sawa, ndiyo maana zipo imani zinazomuona mungu wao hata kwa macho yao ya nyama hapahapa duniani. Suala ni kuamini huyo mungu kwanza halafu juu ya ukweli wake au uongo wake ni hatua ya pili. Kwamfano bila kuamini na kujua kuwa kuna mtu anayeitwa JBC wa USA huwezi kunitofautisha naye ungejua mimi ndiye.Imanininaweza kuwa yavjweli au uongo.
Unaweza kuamini kwamba wewe ni James Brien Comey, aliyekuwa Mkurugenzi wa 7 wa FBI.
Lakini, kuamini hivyo kunakufanya wewe uwe James Brien Comey, Mkurugenzi wa 7 wa FBI?
Na unajuaje kwamba "hapa naamini mimi ni James Brien Comey, Mkurugenzi wa 7 wa FBI" kimakosa, mimi ni Mtanzania tu ambaye huyu James Brien Comey namuina kwenye TV tu. Na hapa mimi ndiye kweli huyo James Brien Comey mwenyewe?
Kifupi, imani inaweza kuwa ya ukweli au uongo. Unajuaje hii imani ya ukweli na hii ya uongo?