Pre GE2025 Mara: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Mara: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WanaJF,​

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Mara. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mara.jpg

Mkoa wa Mara uko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, una historia tajiri na ya kipekee inayohusisha makabila mbalimbali, harakati za uhuru, na urithi wa kihistoria wa ukanda wa Ziwa Victoria. Mkoa huu hukaliwa na makabila ya Wakuria, Wajita, Waluo, Wazanaki, Waisenye, na Wagusu

MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA MARA
Katika muhtasari wa maeneo ya utawala, mkoa huu una halmashauri ambazo zimegawanyika katika mamlaka za miji na wilaya.

Idadi ya Watu
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Mara ni 2,372,015; wanaume 1,139,511 na wanawake 1,232,504, yenye jumla ya wilaya 7.

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi
Mkoa wa Mara una jumla ya Majimbo ya uchaguzi Kumi
  • Jimbo la Musoma Mjini
  • Jimbo la Musoma Vijijini
  • Jimbo la Rorya
  • Jimbo la Butiama
  • Jimbo la Bunda Mjini
  • Jimbo la Bunda
  • Jimbo la Serengeti
  • Jimbo la Tarime Mjini
  • Jimbo la Tarime Vijijini
  • Jimbo la Mwibara
HALI YA UCHAGUZI MKUU 2020

Hayati John Magufuli kupitia CCM alipata kura nyingi, akishinda kwa zaidi ya asilimia 80.

Katika Ubunge, CCM ilifanikiwa kushinda majimbo yote, huku CHADEMA ikipoteza baadhi ya ngome zake muhimu kama jimbo la Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Bunda

Kwa upande wa udiwani, CCM pia ilishinda kata nyingi, na kufanya mkoa wa Mara kuongozwa zaidi na chama tawala kwenye ngazi zote za kisiasa.

Kama ilivyo kwa udiwani sehemu kubwa nchini, pia kwa mkoa wa Mara Vyama vya Upinzani vilipata changamoto za wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Updates
January
February
March
ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Back
Top Bottom