Baadhi ya mitaa katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara, wamelalamikia kutokuonekana na kusomeka vyema kwa majina yao katika orodha ya wapiga kura huku wakisema hali hiyo inachangia kuchelewesha zoezi la upigaji kura na watu kuendelea na majukumu yao.
Wapiga kura hao wanadai wamefika vituoni mapema, lakini muda mwingi wameupoteza katika kutafuta majina ambapo wamezishauri mamlaka husika kuhakikisha changamoto hiyo haijorudii wakati mwingine.