Mara: Watu tisa wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba walizokuwa wakiishi kusombwa na maji

Mara: Watu tisa wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba walizokuwa wakiishi kusombwa na maji

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
H
Screenshot 2024-11-25 143508.png


Hii inasikitisha sana wakuu, maumivu ya hapo hayaelezeki kwa kweli.

========

Watu tisa wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba walizokuwa wakiishi kusombwa na maji baada ya mto uliopo jirani na makazi yao kujaa maji, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Tarime.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Novemba 25, 2024 katika Mtaa wa Bugosi, Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara ambapo miili ya watu hao ilisombwa hadi ndani ya mto Mori uliopo jirani na makazi yao.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Edward Gowele amesema hadi sasa miili saba imekwishaopolewa kutoka mtoni na utafutaji wa miili mingine unaendelea kwa kushirikisha vyombo vya uokoaji na wenyeji wa eneo hilo.

Amesema katika tukio hilo watu wawili wamenusurika ambapo mbali na vifo hivyo, pia limesababisha uharibifu wa mazao yaliyosombwa na maji hayo na mali.
 
Back
Top Bottom