Mara ya kwanza kumiliki simu yako binafsi ya mkononi

pangakali 2

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
239
Reaction score
221
Habarini za asubuh wakuu.

Tukumbuke nyuma kidogo. Nakumbuka mara yangu ya kwanza kumiliki simu ilikua mwaka 1999 nilikua mwanza nikiwa kwenye daladala mara pap naona simu kwenye siti tulivyofika nyakato nikawa wa mwisho kushuka jasho linanitoka balaa. Nikawaza kuitangaza nikaona itakua halali ya Kondatka. Nikajipa moyo kuwa sijaiba atakaye jitokeza nitampatia.

Nimekaa nayo mwaka mzima ndani bila kuitumia. Matokeo ya darasa la saba yalivyotoka nikaenda kuanza form one Wilaya fulani Mkoa wa Kigoma. Kwa kipindi iko matumizi ya simu za mkononi yalikua bado hayajafika. Tukiwa form two Voda wakazindua mawasiliano. Hapo ndio nilianza kuitumia rasmi kwa mara ya kwanza. Kwa kweli ilinisaidia sana kupata pata vijisent kwa ajili ya kujikimu. Kwa waliokuwa wanahitaji kubip nilikua nawatoza sh 50, kutuma ujumbe 100.

Je? Ewe mwana JF mwenzangu ulimiliki simu yako kwa mara ya kwanza mwaka gani na uliipataje?


 
2009 baada ya kuiba simu ya mzee vodafone ambayo alikua haitumii nikawa naitumia kwa kificho. Kuna siku kaitafuta sana kaikosa akicheki kwene kiboksi kuna risiti tu na charger simu haipo [emoji23] akatoka kwa hasira akasema yeyote anaejijua kachukua simu yangu arudishe mwenyewe hapo natetemeka nikaipeleka nilishangaa hata hakufoka kesho yake akaniita akanikabidhi rasmi.
 
Ukajifunza nini baada ya hapo mkuu
 
Inafurahisha na kufundisha pia
 
Mwaka 2007. Nokia 3100 nilipewa na mzee kama zawadi ya kufaulu std 7. Ilikua bado mpya kabisa .
 
Big up mkuu. usisahau kurudisha fadhira kwa mzee kama alivyokuthamini by that time
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…