Nilipigana na house girl mmoja hivi ambae umri wetu ni mmoja. Ilikuwa mwaka huu mwezi wa tano, chanzo kikiwa ni rafiki yangu wa damu. Tukio hilo lilinichafua sana na kushangaza watu, maana mie ni mpole na sina makuu na mtu. Kwa kweli sitasahau maishani mwangu na sitataka kuwa karibu na marafiki tena. Mwaka 2017 utakuwa ni mwaka wa mabadiliko kwangu, sihitaji rafiki yeyote aguse maisha yangu kwa namna yoyote ile. Nitabaki kuwa mimi kama mimi nikijenga ushirikiano wa kutosha na Mungu wangu pamoja na kazi yangu pekee. Yaliyotokea mwaka huu sihitaji yajirudie tena katika maisha yangu yaliyosalia chini ya jua.