Mara ya Mwisho Mzee Waikela Aliponitembelea 2018

Mara ya Mwisho Mzee Waikela Aliponitembelea 2018

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MARA YA MWISHO MZEE WAIKELA ALIPONITEMBELEA 2018

''Kauliza mwenye kuuliza, ''Inaelekea unampenda sana Mzee Waikela.''

''Hakika nampenda. Vipi nisimpende Bilal Rehani Waikela ilhali alipendwa na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir?''

Ilikuwa tarehe kama ya leo Mzee Waikela alipokuja kunitembelea nyumbani.

Ilikuwa asubuhi na mapema kiasi cha mtu kuanza kusali Dhuha.

Nakumbuka katika mazungumzo yetu aliniambia kuwa nakala mbili ya vitabu vya Abdul Sykes nilivyompa Morogoro tulipokwenda kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda vilipotea pale pale mjini.

Basi nikampatia nakala nyingine mbili.

Mzee Waikela alikuwa amefika jana yake kutoka Tabora kaja Morogoro kumtia moyo Sheikh Ponda katika kesi zilizokuwa zikimkabili moja ikiwa ni ya kiwanja cha EAMWS kilichokusudiwa kujengwa Chuo Kikuu Cha Waislam.

Mimi nilifika asubuhi na kwa bahati mbaya nikakuta lango kuu la mahakama limefungwa na askari wametanda nje kwa kuwa palitokea vurugu na kutoelewana kati ya polisi na Waislam.

Kisa ni kuwa Muislam alipiga ''Takbir,'' iliyoitikiwa ''Allahu Akbar.''

Hii ikasababisha hofu kwa askari na haraka wakafunga lango na kuwazuia Waislam kuingia ndani ya viwanja vya mahakama.

Huu ulikuwa mwaka wa 2015.

Nilimwendea askari mmoja ambae ndiye aliyekuwa mkubwa hapo na nikamuomba aniruhusu kuingia mahakamani.

Alinikatalia na nilipomsihi na kumweleza kuwa mimi natoka Dar es Salaam nimesafiri hadi Morogoro kwa nia ya kumjulia hali Sheikh Ponda ambae nilimtambulisha kuwa ni ndugu yangu niliruhusiwa kupita.

Picha hizo hapo chini utaona askari wametanda langoni.

Baada ya kukutana hapa mahakamani Morogoro ndipo ikapita miaka mitatu na mwaka wa 2018 Mzee Waikela akaja Dar es salaam na kufika nyumbani kunijulia hali tukapiga hiyo picha hapo chini.

Lakini tulikuwa sote mahakama ya Kisutu kwenye kesi ya kiwanja cha EAMWS ambako yeye alikuwa shahidi.

Mzee Waikela alikuwa na kawaida kila mtu akimwambia kuhusu kuandika maisha yake jibu lake lilikuwa, "Mohamed kaeleza historia yangu katika kitabu cha Abdul Sykes aliyoandika kuhusu mimi yanatosha."

1657920446152.png
1657920491984.png
1657920515574.png
1657920540471.png
1657920563519.png
 
Back
Top Bottom