Mara ya mwisho....

Mara ya mwisho....

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Mara ya mwisho kumsifia mke/mume/mpenzi wako ilikua lini?!

Kumsifia mwenzi wako haswa mkiwa faragha kuhusu mwili wake/sura/umbo/sauti n.k kunaongeza kujiamini kwake.Fikiria mwanamke ambae hata wakati wa kuvaa nguo anajifunika na taulo au anafunga kabisa mlango na komeo wakati wapo wawili tu ndani ya nyumba hata kukiwa na tatizo kwenye sekta ya mapenzi ataanzia wapi kumweleza mwenzake na kumwaga hisia zake?! Mwanaume ambae nae anavua na kuvalia humo humo bafuni ili mwenzie asimuone anawezaje kueleza mapungufu yao iwapo yatajitokeza kwenye sekta ya mapenzi?!

Mjengee mwenzako kujiamini kwa kumsifia na kumjulisha kwamba unapenda alivyo...hata kama ni kibonge sana...kimbaumbau...ana makovu...ana kitambi au ana ukilema wa aina yoyote ile.Mfanye ajisikie vizuri awapo na wewe...mfanyie ajisikie huru bila aibu/woga mbele yako...mfanye ajisikie amani na pia furaha.Mwonyeshe mtazamo chanya juu ya muonekano wake ili ajiamini. Na kama kuna kitu ambacho unadhani kinahitaji kurekebishwa (achana na kuongeza viungo kwa madawa ya mchina) kama kupunguza mwili mshawishi vizuri kwa upendo afanye hivyo ili na wewe uweze kutidhika nae pia kumfurahia.
 
Wewe Lizzy Licious mara ya mwisho kusifiwa kuhusu mwili wako/sura/umbo/ na sauti yako ilikuwa lini? Na wewe kumsifia mwenzako mara ya mwisho ilikuwa lini?
 
Wewe Lizzy Licious mara ya mwisho kusifiwa kuhusu mwili wako/sura/umbo/ na sauti yako ilikuwa lini? Na wewe kumsifia mwenzako mara ya mwisho ilikuwa lini?
Ungejibu kabla hujaniuliza mimi ningefurahi sana...
 
Mtoto shoo kaa wewe bado tu hujapata anayekugusa mtima? Unbewivable!!!
Hehehe...nimesema sijapata NAFASI YA KUMSIFIA sio sijapata wa kumsifia.Back to topic....naomba uchangie basi tuendelee.
 
Hehehe...nimesema sijapata NAFASI YA KUMSIFIA sio sijapata wa kumsifia.Back to topic....naomba uchangie basi tuendelee.

Alaaa kumbe ndo hivyo. Haya bana...ila ujue ukiujua huu ule huuwezi utachoka miguu kwa utembezi.....
 
Naogopaga mke wangu kuona Biology yangu...Liizy leo tu nimemwambia bibie...wewe mzuri katoa sauti ya kile kicheko cha taarabu...nikanyamaza kimya....sitajaribu tena kusifia...
 
ukikasoma haka katoto (Lizzy) utagundua kenyewe kako demanding na kanapenda 'kufanyiwa' na sio kufanya...

it is complicated and very strange how one can be such demanding ... pole kwa bhana 'ake!!
 
loh kusifiwa kuzuri jamani t usifiane
tupeane zawadi
tukumbatiane
kiss in foreheads...showing tht we are cute
kiss in the lips showing tht we love each
kiss in the neck showing tht we are real friends....
ni vuzuri kusifu na kusifiwa
 
Usikate tamaa magulumangu. inawezekana kacheka kama Sarai alipoambiwa utapata mtoto (she was shocked and didnt believe). Kama huna mazoea ya kumsifia sio lazima kwa sura tu, kuna nywele, macho, pua, kucha, vidole na yale mengine ya chumbani. hata kumsifia mkeo/mwenza kwa kuwa msafi na kuwajibika inatosha kabisa kumfanya ajisikie kuthaminiwa. Kwa mfano ww mkeo akuambie ''magu, u ar a good and responsible man. asante kwa kututunza mimi na watoto. na kwa kutupenda na kutujali'', hata kama ww sio handsome bado utajiskia ka-handsome flani,lol!

Naogopaga mke wangu kuona Biology yangu...Liizy leo tu nimemwambia bibie...wewe mzuri katoa sauti ya kile kicheko cha taarabu...nikanyamaza kimya....sitajaribu tena kusifia...
 
Very Useful post... Hio ni moja ya kitu ambayo husaulika kwa wenza...
 
mmmmmmh, duh...................najuta kusifia,maana nilikuwa namsifia akajihisi malaika na mimi ni kibwengo tu....akanikimbia!

Lakini zoezi nimelianza jana kwa kukusifia kwa michango yako, sasa kwenye umbo,sura,muonekano............mpaka nikuone au kama unafanana na avatar yako................niambie nianze kushusha misifa.
 
Sasa wewe ni mlw...sante kwa kutukumbusha..'mke huisikia sauti ya huba ya mume na mme huyafurahia matendo mema ya mkewe'
 
Kwanza,wenza si vyema kuwa wanaoneshana maungo yao mara kwa mara,kwani inaweza kusababisha kukinai!Pili kwa mtu mwenye kuijua thamani ya mke/mume hawezi kumsifia kwa umbo/rangi au mambo ya kuonekana kwani mambo hayo ni ya mwilini na kama umekua na huyo ulienae kwa misingi hiyo matatizo yako jirani,usisubiri mpaka ujengewe kujiamini na mtu mwingine nje yako,jiamini mwenyewe!Kama unashindwa kujiamini mbele ya mke/mume wako,hufai kuwa na wadhifa huo!
 
Back
Top Bottom