Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Mara ya mwisho kumsifia mke/mume/mpenzi wako ilikua lini?!
Kumsifia mwenzi wako haswa mkiwa faragha kuhusu mwili wake/sura/umbo/sauti n.k kunaongeza kujiamini kwake.Fikiria mwanamke ambae hata wakati wa kuvaa nguo anajifunika na taulo au anafunga kabisa mlango na komeo wakati wapo wawili tu ndani ya nyumba hata kukiwa na tatizo kwenye sekta ya mapenzi ataanzia wapi kumweleza mwenzake na kumwaga hisia zake?! Mwanaume ambae nae anavua na kuvalia humo humo bafuni ili mwenzie asimuone anawezaje kueleza mapungufu yao iwapo yatajitokeza kwenye sekta ya mapenzi?!
Mjengee mwenzako kujiamini kwa kumsifia na kumjulisha kwamba unapenda alivyo...hata kama ni kibonge sana...kimbaumbau...ana makovu...ana kitambi au ana ukilema wa aina yoyote ile.Mfanye ajisikie vizuri awapo na wewe...mfanyie ajisikie huru bila aibu/woga mbele yako...mfanye ajisikie amani na pia furaha.Mwonyeshe mtazamo chanya juu ya muonekano wake ili ajiamini. Na kama kuna kitu ambacho unadhani kinahitaji kurekebishwa (achana na kuongeza viungo kwa madawa ya mchina) kama kupunguza mwili mshawishi vizuri kwa upendo afanye hivyo ili na wewe uweze kutidhika nae pia kumfurahia.