Mara yangu ya kwanza kumtia machoni Iddi Simba 1980s

Wadogo zangu walikuja kunitembelea likizo, kama ilivyo ada kila mwaka miaka hii ya karibuni.

Basi wakaniuliza, kaka mkubwa tukuletee zawadi gani? Swali tata sana hili.

Nikaomba waniletee asali ya Tanzania na kitabu cha Mkapa.

Kitabu kilikuwa "out of print", zikapigwa simu mpaka kikapatikana, nikaletewa.

Nikakisoma kwa hamu, kwa kituo. Kwa jicho la mtu anayeijua familia ya Mkapa si kwa kupitia magazeti na siasa, bali kama mtu niliyekua na watoto wa familia Upanga.

Kusema kweli, Mzee Mkapa katupiga chenga tu na hiki kitabu. Ni muhimu kukisoma, lakini kwa caliber ya muandishi kama yeye, alichofanya kwenye kitabu hiki ni kutoa muhtasari wa mambo machache tu, na hata hayo kayaongelea kijuu juu tu.

Mfano, alivyoelezea jinsi alivyoingizwa kingi kwenye issue ya EPA, yani ukisoma unaona kabisa hapa mshua anatumia kitu kinaitwa "plausible deniability". Mkapa ni mtu meticulous sana, sana tu, na si mtu wa kudanganywa kitoto vile.

Ila, naona kaona afadhali apate fedheha ya kujifanya alikuwa mjinga, kuliko kupata lawama ya kwamba alikuwa "fisadi".

Ni kitabu kizuri kama unataka kujua historia ya maisha ya awali ya Mkapa, ingawa hata kwenye familia nako ameshindwa hata kumtaja Peter kama mtoto wake wa kufikia, ukisoma utafikiri Nick na Stephan ndio watoto pekee, lakini kama unataka kujua mambo kwa undani, Mkapa kabakisha maneno mengi sana kuliko aliyoandika. Kuanzia alivyokuwa anamwambia Nyerere kwamba Kambona anamsengenya, na Nyerere akiwa haamini anam dismiss Mkapa, mpaka ukweli kuhusu alivyokubali kupiga dili la EPA.

Kabla ya kusoma kitabu cha Mkapa, nilikuwa nasoma kitabu cha balozi wa serikali ya Marekani chini ya Obama hapo UN, Samantha Power, kinaitwa "The Education of An Idealist: A Memoir". Ukisoma wenzetu wanavyozama katika kueleza maisha yao na maamuzi waliyochukua wakiwa madarakani, halafu ukasoma kitabu cha Mkapa, utaona kitabu cha Mkapa kimejaa habari za "danganya toto, kula kunde, nyama mbichiii".

The book is full of plausible deniability, omissions,obfuscation, conveniently late conversions to being a democrat, the list goes on.

In short, the book is an insults to our collective intelligence.
 

..siku ya uzinduzi nilimuona Mzee Mramba.

..Je,Mzee Mkapa amezungumzia lolote kuhusu kesi ya Mramba na Yona?

..amezungumzia kuhusu kesi ya Prof.Mahalu ambaye alilazimika kwenda kumtetea?

..vipi kuhusu lawama za muda mrefu kuhusu mikataba ya madini? ametoa neno kuhusu masuala hayo?
 
Kitabu kizima sikumbuki kuona Mramba katajwa.

Amemtetea sana sana tu Dr. Mahalu, ukikisoma kitabu ndiyo utajua kuwa Mkapa na Mahalu ni maswahiba wakubwa sana, nilikuwa najua ni marafiki, lakini kusoma kitabu kumenifungua macho kujua kwamba wanapatana sana.

Hayo mambo ya madini kaongelea in passing juu juu tu. Unasoma unaona boilerplate tu.

Nilitaka kuandika full review hapa, lakini nikataka kusubiri muda kidogo labda watu wengine watapata kukisoma niweze kujadiliana na watu wengine waliokisoma pengine nakosea, huwa najipa nafasi ya kuweza kukosea siku zote.
 

..kama Mkapa anajivunia kwa ku-turn around the economy lazima awaseme vizuri mawaziri wake wa fedha ambao ni yona na mramba.
 
Asilimia kubwa la hili jukwaa la HISTORIA ni kama watu wamekuachia ww (mo saidi)...hongera lakini kwanini na katika maisha yako hujawahi kukutana na MKRISTO aliyefanya jambo nzuri kijamii ya tanganyika/Tanzania uje usimulie humu...maana naona wote isipokuwa nyerere ni waislamu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Emanuel...
Niruhusu kujibu swali lako kwa kukuuliza swali.

Mbona hawa unaowasoma hapa hawakupata kutajwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Emanuel...
Niruhusu kujibu swali lako kwa kukuuliza swali.

Mbona hawa unaowasoma hapa hawakupata kutajwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa maana hiyo, jee hakuna Wapigania Uhuru wenye imani ya Kikristo ambao hawakutajwa? Wewe ukubali tu ni mdini. Hilo ni jambo lisilopingika na usilete kauli zako za kijanja kukwepa.
 
Hapa alikuwa ameisha acha kupiga masanga?
 
MS, tuletee anecdotes aka story za Abdulrahman Babu kama unazo.
 
Kwa maana hiyo, jee hakuna Wapigania Uhuru wenye imani ya Kikristo ambao hawakutajwa? Wewe ukubali tu ni mdini. Hilo ni jambo lisilopingika na usilete kauli zako za kijanja kukwepa.
Ndjabu...
Sina tatizo mtu ananiitaje.

Wala sina "kauli ya ujana," wengi wananisoma kwa yale ninayoandika yanayovutia usomaji na huu si, "ujanja."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MS, tuletee anecdotes aka story za Abdulrahman Babu kama unazo.
Ndjabu...
Iko siku nilishinda kutwa nzima na Abdulrahman Babu London pamoja na Ahmed Rajab.

Tulianza safari yetu Brixton siku hizo palitokea machafuko makubwa kwenye kitongoji hicho.

Ngoja nitafute shajara zangu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chief Kiranga

Upo makini sana Mkuu
Ila jambo moja tu
Kukataa uwepo wa Muumba wako
Hili linakuzamisha topeni kabisa Chief
Barikiwa sana
Mola atuongoze njia ya sawa
Ila upo makini Bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chief Kiranga

Upo makini sana Mkuu
Ila jambo moja tu
Kukataa uwepo wa Muumba wako
Hili linakuzamisha topeni kabisa Chief
Barikiwa sana
Mola atuongoze njia ya sawa
Ila upo makini Bro

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijakataa kuwepo kwa muumba wangu.

Siku zote nimekuwa nikisisitiza muumba wangu kuwepo.

Mmoja ni Baba yangu mzazi, mwingine ni Mama yangu mzazi.

Kama unaweza kuthibitisha mwingine yupo, thibitisha.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…