Mara zote nimetumia kinga

Mara zote nimetumia kinga

Red Scorpion

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,736
Reaction score
4,252
ALITOKEA MVULANA MMOJA:

MVULANA: Daktari, rafiki yangu wa kike ni mjamzito, lakini mara zote nimekua nikitumia kinga. Inawezekanaje hii?

DAKTARI: Ngoja nikusimulie hadithi. Kulikua na Muindaji ambaye alikua anabeba bunduki kila aendako. Siku moja, alichukua mwamvuli badala ya bunduki na akaenda nayo. Ghafla akatokea Simba mbele yake. Ili amtishie Simba, muindaji akatumia mwamvuli na kummiminia risasi Simba. Simba akafa palepale!

MVULANA: Sio kweli!! Lazima kulikua na mtu mwengine pembeni aliyempiga risasi Simba.

DAKTARI: Nashukuru umeelewa somo!!
 
Back
Top Bottom