Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
MARADHI 13 MAKUBWA YANAYOWASUMBUWA WA-TANZANIA
(1) SHINIKIZO KUBWA LA DAMU/KITAALAMU HIGH BLOOD PRESSURE
Maana ya Shinikizo kubwa la Damu: Ni ongezeko la nguvu ya msukumo wa
damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda
kwenye viungo na tishu mwilini.
Ukubwa wa shinikizo hilo la damu utegemea wingi na nguvu ya msukumo
wa damu kutoka kwenye moyo na ukubwa wa mishipa inayopeleka damu mwilini.
Kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu mwilini ni 120/80mmHg au
chini yake. Pale kiwango kinapokuwa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo huwa
ni shinikizo kubwa la damu.
Dalili: Kwa kawaida hakuna dalili za wazi zinazojitokeza pale ambapo una
shinikizo kubwa la damu. Utafahamu kama una shinikizo kubwa la damu
kwa kupimwa na mtaalamu katika kituo cha tiba. Endapo shinikizo lako la
damu litakuwa liko kiwango cha juu sana unaweza:
Ukaumwa kichwa mara kwa mara hasa sehemu ya kisogo
Kutokwa na damu puani
Ukapata kizunguzungu
Kupata maumivu ya kifua
Moyo kwenda kasi wakati umepumzika
Kushindwa kufanya mazoezi kwa kushindwa kupumua
Kusikia mapigo ya moyo wako wakati umepumzika
Na kupata uchovu wa mara kwa mara.
Muda wa tatizo: Kwa bahati mbaya watu wengi huishi na tatizo hili kwa
muda mrefu bila kufahamu kwani hakuna dalili zilizo bayana. Mara nyingi
shinikizo kubwa la damu hutambulika pale unapokwenda kituo cha huduma
ya afya kupima afya yako au kupata matibabu ya tatizo jingine la kiafya.
Hali hii humweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo hivyo ni
muhimu kuwa na tabia ya kupima afya yako mara kwa mara.
Sababu: Sababu hasa za shinikizo kubwa la damu kwa sehemu kubwa
hazijulikani. Hata hivyo shinikizo la damu hubadilika mara kwa mara
kutegemeana na shughuli mtu anayofanya, hali ya joto, chakula
alichokula, hali ya msongo wa mawazo, ukiwa umelala au kusimama na
hata matumizi ya baadhi ya dawa.
Watu wenye umri wa miaka 45 au zaidi wako kwenye hatari zaidi ya kupata
shinikizo kubwa la damu kutokana na mabadiliko yanayotokea katika
mishipa yao ya damu. Vilevile mafuta, lehemu au madini ya chokaa yakizidi
mwilini huwa na tabia ya kujikusanya katika kuta za ndani za mishipa ya
damu kidogo kidogo na kusababisha mishipa hiyo kuwa nyembamba na
hivyo kupunguza uwezo wake wa kutanuka. Hali hii huchangia kwa kiasi
kikubwa kupata shinikizo la damu.
Viashiria vya shinikizo kubwa la damu: Mambo yanayoongeza uwezekano
wa kupata shinikizo kubwa la damu ni pamoja na:
Kuwa na historia ya shinikizo la kubwa la damu katika familia yako
Kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40
Kuwa na jinsia ya kiume (huwapata wanaume zaidi kuliko wanawake)
Kuwa na uzito uliozidi kiasi (kwa kawaida uzito unaotakiwa ni kilo 70)
Kuwa na msongo wa mawazo (stress)
Kuwepo na matatizo mengine ya kiafya mwilini, kama magonjwa ya figo,
matatizo ya mishipa ya damu, magonjwa ya moyo, kisukari au saratani
Matumizi ya chumvi kwa wingi au vyakula vyenye chumvi nyingi
Matumzi ya baadhi ya dawa
Utumiaji wa pombe na uvutaji sigara
Ujauzito
Nifanye nini kujiepusha na shinikizo kubwa la damu?
Epuka vyakula vyenye mafuta mengi na chumvi nyingi
Epuka mafuta yenye asili ya wanyama
Epuka kuwa na uzito uliozidi
Punguza kula nyama hasa nyama nyekundu
Epuka matumizi ya pombe, sigara na tumbaku
Kudhibiti msongo wa mawazo
Fanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku
Madhara ya shinikizo kubwa la damu
Magonjwa ya moyo(moyo kuwa mkubwa, moyo kushindwa kufanya kazi)
Magonjwa ya figo
Uharibifu wa macho na kushindwa kuona
Kisukari
Kiharusi (Stroke)
Kifo
Matibabu:
Fuata ushauri wa daktari ikiwa ni pamoja na kutumia dawa kama ulivyoelekezwa. Mara nyingi wagonjwa wa shinikizo kubwa la damu huacha
kutumia dawa wanapohisi nafuu. Hii si sahihi kwani huongeza uwezekano wa kupata madhara.
Epuka vyakula vyenye chumvi nyingi.
Epuka mafuta mengi
Punguza kiasi cha nyama nyekundu
Punguza au epuka matumizi ya pombe
Kula matunda na mbogamboga kiasi cha kutosha katika kila mlo.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Herbalist MziziMkavu