Maradhi ya moyo huua watu milioni 18 duniani kila mwaka

Maradhi ya moyo huua watu milioni 18 duniani kila mwaka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Watu milioni 17.5 hufa kutokana na maradhi ya moyo duniani kila mwaka, daktari bingwa wa tiba na upasuaji wa moyo nchini, Marehemu Dk. Ferdinand Masau, amesema.


RIP. Dk. Masau amesema kati ya watu hao wanaokufa kwa maradhi hayo, milioni 8.5 ni wanawake.


Amesema tishio hilo la vifo kutokana na ugonjwa huo limemsukuma kutunga vitabu viwili vinavyoelezea namna maradhi hayo yanavyotokea na jinsi ya kuyatibu kabla hali haijawa mbaya.


Amesema vitabu hivyo vimeandikwa kwa lugha ya Kingereza na kingine kwa lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha watumiaji wa lugha zote mbili kutumia vitabu hivyo kupata elimu itakayowasaidia kufuatilia afya zao.


“Mtu akisoma vitabu hivi atajua dalili za maradhi mbalimbali ya moyo, namna ya kuyazuia na namna ya kuyatibu kabla hali haijawa mbaya, watu wengi wanakufa ghafla kwakuwa hawana kawaida ya kufuatilia afya zao, vitabu hivi vitakuwa msaada mkubwa kwa Watanzania,” alisema Dk. Masau ambaye ni mwanzishili na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo Tanzania (THI).


Alisema nafsi yake imemsukuma kuandika vitabu hivyo baada ya kuona maradhi ya moyo ndiyo yanayoongoza kwa kuua watu wengi duniani, wakati vifo vingine vingeweza kuzuilika iwapo wahusika wangewahi matibabu.


“Watu wengi wanakufa ghafla, mtu anahudhuria mkutano unasikia kafa kikaoni lakini ukichunguza tatizo lililomuua halijaanza ghafla, angekuwa na utamaduni wa kufuatilia afya yake angejua dalili mapema na akajitibu maana dalili za maradhi ya moyo ziko wazi kabisa,” alisema.


Dk. Masau alisema homa zinazosababishwa na wadudu wanaosababisha vidonda vya kooni na homa (rheumatic fever), baada ya muda husababisha madhara kwenye moyo (rheumatic heart disease na kwamba homa hizo mara nyingi huwapata watoto wa umri kati ya miaka 5-15.


Alisema maradhi hayo huwapata hasa walioko kwenye mazingira ya umaskini ambayo ni pamoja na kuishi katika msongamano, kutokuwa na nyumba bora, lishe duni na ukosefu wa huduma bora za afya.


Alisema kutokana na matatizo hayo kukithiri, sasa ni wakati mwafaka kwa wasomi na wataalamu kutumia elimu waliyoipata kuelimisha umma kuhusu maradhi ya moyo kwa njia mbalimbali ikiwemo kuandika vitabu.


Alisema vitabu hivyo vinaweza kutumika kuwaelimisha wataalamu wa afya ili wajue namna mbalimbali za kuwatibu wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.
Maradhi ya moyo huua watu milioni 18 duniani kila mwaka
 
Marehemu Dk. Ferdinand Masau ni asset iliyopotea,mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.Maandiko yake yatadumu daima na milele!
 
Back
Top Bottom