Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
Utangulizi
Binadamu mwenye afya bora ya mwili na ya akili huzaliwa kutoka kwa watu (mwanamme na mwanamke) wenye afya bora. Miezi mitatu hadi sita kabla na kipindi chote cha ujauzito, ni muhimu baba na mama (hasa mama) kuhakikisha wana afya njema, na wanakula Milo kamili. Bahati mbaya, watu wengi hawafanyi maandalizi kama haya. Mama anashika ujauzito huku akiwa anakula chakula kisichokuwa na virutubisho vya kutosha. Wengine wanakunywa pombe kupindukia, wanavuta sigara na/au kutumia madawa ya kulevya. Tabia hizi, kabla na kipindi cha ujauzito husababisha baadhi ya watoto kuzaliwa wakiwa na matatizo ya kiafya, ikiwa ni pamoja na ulemavu.
Uwiano wa Uzito na Urefu
Kuna kikokotoo kinachoonyesha kama MTU ana uzito unaofaa au la; ambacho ni uzito (kg), ukigawanywa kwa urefu wake katika mita za mraba (kg/m²), ambapo mtu mwenye uzito wa kawaida ana kipimo cha kati ya 18.5 na 24.9 kg/m².
Sheria/Kanuni Nane za Afya:
Kanuni za uponyaji wa asili zinafanya kazi na jitihada za mwili kurejesha afya yake, Vance Ferrell na Harold M. Cherne (2009). Ikiwa MTU atakuwa mgonjwa, ni muhimu kujua chanzo. Ni lazima hali ya ugonjwa ibadilishwe, ikiwa ni pamoja na kubadili tabia zisizo sahihi.
1. Hewa unayovuta. Bila hewa, MTU anakufa. MTU au mmnyama anaweza kuishi kwa wiki moja au zaidi bila chakula, na siku kadhaa bila maji, lakini bila hewa anaangamia ndani ya dakika chache. Mamilioni ya watu wanaugua maradhi mbalimbali kutokana kutopata hewa (oksigeni) ya kutosha. Ili kuwa na afya bora, ni lazima tupumue vizuri. Hewa safi, inayojaza mapafu oksigeni, husafisha damu, na kufanya viungo vya mwili kupata damu safi; hivyo mwili mzima kuwa na afya bora. Upungufu wa hewa safi, hupelekea damu kuwa chafu, na hivyo kuathiri sii tu mapafu, bali pia tumbo, maini, ubongo, mmeng'enyo wa chakula, ngozi, moyo, na maeneo mengine; Kila seli ya mwili ni lazima ipate oksigeni ya kutosha wakati wote, vinginevyo, itakuwa dhaifu na kufa. Vance Ferrell na Harold M. Cherne (2009).
2. Mwanga wa jua kwenye mwili wako. Kwa mujibu wa Vance Ferrell na Harold M. Cherne (2009), kuna mamilioni ya seli nyekundu zinazozunguka kupitia mishipa midogo ya damu katika kila eneo la inchi za mraba 3,000 la ngozi yako. Na kuna tezi ndogo za mafuta katika ngozi ambazo kitaalam zinaitwa ''Sterols''. Hizi zinapapigwa na mwanga wa jua, kuna vitu vinavyojulikana kama ''ergosterols'' vinanururushwa na kubadilishwa kuwa vitamin D: hii ni muhimu mwilini, inakuwezesha kuwa na mifupa, meno na kucha imara.
3. Nguvu ya kiasi. Ili kuhifadhi afya, kiasi katika vitu vyote ni muhimu. Ni lazima tuwe na kiasi katika vitu vizuri, na kujizuia kwa vitu vyenye madhara. Tunapaswa kuwa na kiasi katika kufanya kazi, kiasi katika kula na kunywa.
4. Mwili wako unahitaji kupumzika. Wagonjwa wanaolazwa hospitalini au katika vituo vya afya, hulala vitandani mchana na usiku kwa sababu nguvu ya kupumzika ni muhimu katika mafanikio ya kurejejesha afya.
5. Mwili wako unahitaji mazoezi. Kuwa na afya njema, mwili unahitaji mazoezi ya kawaida kama kutembea kwa dakika 30 kwa wakati mmoja mara tatu au nne kwa wiki, ili kukuhakikishia afya njema muda wote. Kwa kufanya mazoezi kwenye eneo la wazi lenye hewa safi, maini, figo, na mapafu huimarika na kufanya kazi yake vizuri. Pia, mazoezi husaidia kuboresha mmeng'enyo wa chakula. Mazoezi, kwa kiasi kikubwa ni bora kwa afya kuliko dawa.
6. Chakula unachokula. Kula kiasi sahihi cha chakula sahihi na kwa wakati sahihi, ni muhimu kwa afya njema. Chakula cha asili walichotumia watu wa kale, na wachache kwa sasa, hasa wale waishio vijijini, ni nafaka (mahindi, ngano, ulezi, mtama, mihogo, magimbi, viazi, nk); mkunde (maharagwe, mbaazi, choroko, dengu, njegere, soya, karanga, korosho, lozi, nk); mboga (mchicha, kabichi, brokoli, bamia, karoti, bitiruti, nyanya, pilipili, vitunguu, nk); na matunda (ndizi, maembe, machungwa, tufaa, matango, parachichi, papai, stafeli, tikiti maji, nk). Vyakula hivi vinavyoandaliwa kwa njia rahisi na ya kiasili, vina afya kwa kiwango cha juu Vance Ferrell na Harold M. Cherne (2009). Kutokana na maandiko ya biblia takatifu, hivi ndivyo vyakula Mungu alivyowapa binadamu wa kwanza, Adam na Hawa.
7. Maji yanayosafisha. Figo zako peke yake huchuja karibu galoni 50 (sawa na karibu lita 227.5 za kimiminika kwa siku. Ndani ya kipindi cha saa 24, zaidi ya lita 8 za sharubati inayomeng'enyeka, humiminika katika njia ya utumbo (''digestive tract''). Mengi ya maji haya, huchakatwa tena na tena na figo zako. Lakini kati ya Lita 2 na 4 hutolewa nje ya mwili kupitia mkojo na mapafu (upumuaji). Kwa sababu hii, kama utakuwa hunywi maji ya kutosha, figo zako hazitaweza kufanya kazi vizuri, na hivyo itasababisha ugonjwa wa figo, Vance Ferrell na Harold M. Cherne (2009). Kwa nyongeza, maji hutoka nje ya mwili kupitia ngozi; kipindi cha joto, au kazi, na mazoezi ya mwili, hukufanya kutoka jasho kwa wingi. Kiasi cha maji kinachotoka kupitia mkojo hupungua kadri mwili wako unatoa jasho kwa wingi.
8. Imani kwa Mungu. Karibu kila MTU ana imani ya dini (Uislamu, Ukristo, Upagani, nk). Watu wote wenye imani hizi tofauti wanaamini uwepo wa nguvu isiyoonekana iliyo juu ya vitu vyote; nguvu hii ndio Mungu! Hii ni nguvu inayotumiwa na binadamu kuleta utulivu wa akili, jambo ambalo linachangia afya ya mwili na akili.
Maradhi Yasiyoambukiza
Kwa mujibu wa tovuti ya wizara ya afya, mnamo tarehe 29, Septemba 2023, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, alisema, takwimu zinaonesha kumekuwa na ongezeko la asilimia 9.4 kwa magonjwa ya Moyo na Shinikizo la Juu la Damu pekee kutoka wagonjwa Mil. 2.5 Mwaka 2017 hadi wagonjwa Mil. 3.4 Mwaka 2022. Taarifa inasema, kutoka mwaka 1980 hadi 2020, shinikizo la juu la damu limeongezeka kutoka 5% hadi 26%; na kisukari kutoka 1% hadi 9%. “Magonjwa haya mawili ndiyo chanzo kikuu cha magonjwa ya Moyo, Figo pamoja na ugonjwa wa Kiharusi''.
Kuelekea miaka 5 hadi 25
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, itengeneze mipango mikakati ya kuhakikisha wananchi wanaishi kwa kuzingatia kanuni za afya nilizozitaja hapo juu. Hii itapunguza kwa kiasi kikubwa wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza, na hivyo kupunguza bajeti inayotengwa kila mwaka kwa ajili hiyo.
Rejea
Vance Ferrell na Harold M. Cherne (2009); ''Natural Remedies Encyclopedia''
www.moh.go.tz

Upvote
2