Maradonna, Platini na Pelle..

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,313
Reaction score
12,170

Kwenye picha ilikuwa ni Mechi ya Hisani iliyoandaliwa Kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya na Rushwa viwanjani!.

Diego Maradona katika mechi hiyo alivaa jezi iliyoandikwa "NO TO DRUGS", Michel Platini alivaa jezi iliyoandikwa "NO TO CORRUPTION" wakati Pelle amesimama kati yao kama mtu wa kati (Neutral party).

Katika kipindi kilichofata cha maisha yao, wachezaji hawa walikabiliwa na tuhuma za kuhusika kwa vitu walivyosimama kupinga!.

Diego Maradona alipigwa marufuku kujihusisha na masuala ya mpira kwa miezi 15 kuanzia mwezi August mwaka 1994 kwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya.

Michel Platini kuanzia mwezi December mwaka 2015 alipigwa Marufuku ya Maisha (Lifetime Ban) kujihusisha na masuala ya mpira kwa tuhuma za rushwa.

Pelle kaendelea baki mtu wa kati (hana tuhuma)!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…