Marafiki wanataka weekend twende kwa Mkapa, nimekataa na kuwaambia najiandaa kwenda kwenye maombolezo tarehe 23

Marafiki wanataka weekend twende kwa Mkapa, nimekataa na kuwaambia najiandaa kwenda kwenye maombolezo tarehe 23

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Habarini waungwana....

Vijana na marafiki zangu wananiambia weekend twende kutazama mechi ya simba, nimewaambia siendi.

Siwezi kwenda kupoteza pesa zangu kwa ajili hiyo, nimewaambia ni heri jumapili nipoe na kusubiri Jumatatu ifike ili niende kwenye maombolezo kwani huko ndipo roho na akili yangu inataka.

Wanasema naenda kujitafutia matatizo, nikasema ni heri hivyo kuliko kwenda kupoteza muda na kupiga makelele kwenye mambo yasiyo na msingi.

Nasubiri muongozo wa maandamano yataanzia wapi ili nifike mapema, sijawahi kushiriki maandamano na hii ni mara ya kwanza.

Naamini vijana tutajitokeza kwa wingi na kupaza sauti kukemea mauwaji na uharamia unao endelea katika nchi yetu.

Tukutane Septemba 23, 2024 DAR ES SALAAM

Soma Pia:
 
Cha muhmu mkuu msivunje sheria na kanuni za nchi tu ,maandamano yawe na tija na c kuharibu ..

Kila la heri mwandamaji shujaaa🙏
Naamini yatakuwa maandamano ya amani, na sitovaa jezi ya chama chochote bali nitaenda kama mtanzania...

Shukran sana mkuu 🙏
 
Back
Top Bottom