Marafiki wengine sio wa kuwatambulisha kwa familia zetu

Marafiki wengine sio wa kuwatambulisha kwa familia zetu

kiroka

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2018
Posts
358
Reaction score
1,887
Ndio tunakutana na marafiki wengi kwenye michakato ya utafutaji riziki wengine tunasaidiana saana ila unamkuta mshkaji katoboa sikio anavaa hereni huyu kumpeleka kwenu kwa maadili ya kwenu nakua mtihani

Au mwana kachora tatoo kwetu huu ni uhuni kiwango cha lami nawezaje kwenda na wew kwa mama angu, .

Inawezakana kabisa kuchora tatoo isiwe uhuni au kuvaa hereni kwa mwanaume isiwe tatizo lakini nikikupeleka nyumbani nikisema wew ni rafiki yangu nitaonekana na Mimi ni mhuni

Unakua na rafiki wa kiume kasuka aisee ni shida
 
Sasa si ukawaambie hao rafiki zako waliofanya hivyo. Unavyotuletea hii report humu sisi tuifanyie nini!?
 
Tatizo letu inaonekana tunaangalia sana muonekano wa nje zaidi ya undani wa mtu.

Ndiyo maana inakuwa rahisi sana kuibiwa na majambazi waheshimiwa wanaovaa suti, halafu kuna watu wana roho safi sana wasuka nywele na wenye tattoo tunawaogopa sana.

Habari hii inanikumbusha mzee mmoja, msomi wa zamani, mtu wa principles zake.

Yule mzee pale jirani na kwake kulikuwa kuna kijiwe wanakaa vijana, kwa mtazamo wake yule mzee, aliwaona wale vijana ni wahuni, wavuta bangi tu, si watu wazuri. Watu wanaokaa kijiweni watakuwaje wazuri? Ni wavivu wasio na kazi tu hawa, alijifikiria.

Siku moja, mzee alikuwa anatoka na gari yake, anawahi mikutano muhimu, gari ikamuharibikia getini kwake.

Sasa, pale getini kwake , upande wa pili wa mtaa ndiyo kuna kijiwe cha wale vijana. Vijana hawakujua kama mzee kiundani anawaona wahuni, wao walimuona huyu mzee wetu wa mtaani tu.

Mzee alikuwa ni wale wazee fulani hawalijui gari zaidi ya kujua kuendesha tu. Kumbe katika wale vijana kuna mpaka mafundi wa magari, wakamsaidia kutengeneza gari chapchap, wakamsukuma, gari likawaka, akawashukuru sana. Akataka kuwapa fedha kidogo, wale vijana wakamkatalia, wakisema kwamba angekuwa mtu mwingine wangechukua, lakini yeye mzee wao wa mtaani wamemfanyia hisani za ujirani tu.

Kuanzia siku hiyo, mzee akawa anasema ameacha kuwadharau watu kwa muonekano wa nje, kwa sababu ameona muonekano mwingine unaficha mambo mengi ya ndani ya mtu.
 
Ndio tunakutana na marafiki wengi kwenye michakato ya utafutaji riziki wengine tunasaidiana saana ila unamkuta mshkaji katoboa sikio anavaa hereni huyu kumpeleka kwenu kwa maadili ya kwenu nakua mtihani

Au mwana kachora tatoo kwetu huu ni uhuni kiwango cha lami nawezaje kwenda na wew kwa mama angu, .

Inawezakana kabisa kuchora tatoo isiwe uhuni au kuvaa hereni kwa mwanaume isiwe tatizo lakini nikikupeleka nyumbani nikisema wew ni rafiki yangu nitaonekana na Mimi ni mhuni

Unakua na rafiki wa kiume kasuka aisee ni shida
Mie nna mwanang ana dread ya kufa mtu alafu ni futi 6 kaenda hewani kinoma alafu ana bonge la mwili yani akipita hapo mbele yako akakwambia nipe simu yako unaitoa bila hata kuuliza lakini ni mtu mmoja mwenye roho nzuri kupitiliza

Unajua kwanin nmemtaja hapa,sababu kama binadam tunahitaji kuwa karibu na kutengeneza urafiki na watu wa kila namna sababu ipo siku utakwama na atakayekuja kukusaidia ni rafiki yako yule wa Tandale na si marioo wa masaki
 
Back
Top Bottom