Marafiki!!!

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Marafiki ni sehemu muhimu sana kwenye maisha ya kila mmoja wetu.Kila siku tunashauriana ishu za mapenzi..tunapeana tahadhari na kushauriana pia kufarijiana ila nadhani swala la urafiki hatulipi uzito ipasavyo!!!

Kama tunavyolipa umuhimu swala la kuchagua nani anafaa kua mpenzi wako ndivyo ilivyo muhimu kuchagua marafiki pia.Kuna aina za marafiki ambao wakati mwingine inabidi tukae mbali nao....marafiki wagomvi, waongo,wafitini, wachonganishi,wambea,wenye wivu kiasi cha kutopenda maendeleo yako, wasio na heshima n.k

Ndani ya wiki mbili nimeshuhudia
.....wasichana wawili wanaoitana marafiki, wanaochekeana wakiwa pamoja wameharibiana mambo yao vibaya sana.

.....Mwingine alikua na tatizo na mwenzake kama watu wazima badala ya kuyamaliza wenyewe akafikisha mpaka taarifa ambazo hazikupaswa kwa mzazi wa mwenzake.Hao ni watu wazima ila bado wanakua kama watoto!!!

.....Mwingine amembeza mwenzake kwamba hana busara.

Kwenye makundi yote hayo matatu hamna heshima ya kweli, urafiki uliojaa mapenzi ya ukweli wala ukomavu wa akili.Siku zote sio vizuri kua rafiki na mtu ambae hajakomaa kiakili sawa na wewe kwasababu ni rahisi sana kutokuelewana nayo inaweza kupelekea chuki inayoweza kuharibu kabisa utu wa mtu....mkaishia kuchukiana maisha!!

Kitu kingine ni kwamba mara nyingi watu unaoonekana nao wanakudefine ulivyo...inawezekana kabisa sivyo ila kama mtu hakufahamu anachukulia kile anachoona au kusikia kuhusu kundi lile la wadada/wakaka kama tabia yako binafsi...kwahiyo kaa mbali na watu usiopenda kuhusishwa nao!

Nwyz nimeona tu tukumbushane umuhimu wa kuchagua marafiki.Kua rafiki na mtu unaeelewana nae lugha...heshimianeni na mpendane.Ukishamwita mtu rafiki yako then unakua na jukumu la kulinda hadhi/sifa ya mwenzako badala ya kuiharibu, kumpa moyo badala ya kumvunja, kumpa faraja badala ya kumpa wakati mgumu, kumheshimu badala ya kumdaharau, kumtunzia siri badala ya kuivujisha n.k.
Tupendane!!

Nawakilisha!!!
 
Asante kwa ushauri mzuri. Tumekuwa tukiwasema vibaya marafiki zetu.
 
nawapenda sana marafiki wa kweli kwa maana 2nasaidia sana ktk matatizo yetu.
 
Asante kwa ushauri mzuri. Tumekuwa tukiwasema vibaya marafiki zetu.
Inabidi tuache!Either unampenda mtu au humpendi...unamheshimu au humheshimu!
 
Jaman naomba niongee ukweli,mm kila nikiona jina la Lizzy humu ndani na post/comments zake I can't control mapigo yangu ya moyo.
 
Jaman naomba niongee ukweli,mm kila nikiona jina la Lizzy humu ndani na post/comments zake I can't control mapigo yangu ya moyo.

Hehehe!Kwanini tena jamani?
 

mpenndwa Lizzy, kwa kweli kwenye jukwaa hili unamudu kila somo. hogera na asante sana.

ila nafikiri nichangie hapo nilipoweka bold kuwa binafsi naamini kuwa marafiki hawachaguliwi, bali hutokea tu maishani mwa mtu kutokana na muingiliano na mtandao (network) wa mawasiliano na watu wengine katika jamii. kama alivyo jirani, rafiki pia hachaguliwi. ni muhimu kuwa mwangalifu na marafiki kwa kujidhibiti hulka na tabia zako wa wale marafiki unaoona mienendo yao si mizuri ili usije kaitumbukiza kwao na kujikuta unaharibikiwa.

ni rahisi kuchagua kazi au mahali pa kuishi, lakini sio rafiki au jirani.

ubarikiwe mpenzi

Glory to God
 
Lizzy sante sana my dear
hata mie nimejifunza mengi..
hopeful many members and visitor
will get a chance to read this.
God bless
 
I love you Lizzy ..
Hii Topic yako imenifanya nitafakari mengi sana be blessed ,Nimemkumbuka rafiki yangu ambaye mungu alimpenda zaidi ya mie nilivyompenda
Kila nikiwaza chozi linanitoka .
 
Nawajali rafiki zangu, huwa ni kimbilio langu la kwanza ninapohitaji ushauri ambao siwezi kuuomba kwa familia.
Ahsante lizzy.
 
Asante Miss Judith...unayosema ni kweli kwamba huwezi kwenda mahali uanze kuchagua yule na yule ila ukishakua karibu na mtu ukagundua kwamba ana tabia usiyopenda sana unaweza kuchagua kuachana na urafiki ule au la!Asante tena kwakuniweka sawa!Be blessed!
 
I love you Lizzy ..
Hii Topic yako imenifanya nitafakari mengi sana be blessed ,Nimemkumbuka rafiki yangu ambaye mungu alimpenda zaidi ya mie nilivyompenda
Kila nikiwaza chozi linanitoka .
Asante mama wa kwanza!I love you too!Pole kwa kumpoteza rafiki yako mpendwa!
Be blessed!
 
Well said Lizzy marafiki ni watu muhimu katika maisha yetu, mimi binafsi nadiriki kusema kusema hapa JF i made friends ambao kwa kweli wamenisaidia sana kimawazo na pia kwa ushauri mzuri wanaonipa hasa pale ninapokuwa nina tatizo fulani kwa kweli nachoweza kusema ni kuwa si cha kuwalipa lakini that bondship niliyonayo na hao marafiki wamekuwa kama ndugu kwangu maana wengine hadi nimeweza kukutana na familia zao nikimaanisha wake zao pia na watoto pia wamenipa ushauri wa kutosha kuhusiana na mambo mbali mbali ya kimaisha
 
well said lizzy, wakati mwingine marafiki ni wa msaada kuliko hata ndugu. tatizo linakuja kama mkijakorofishana halafu akawa hana busara na uvumilivu kama ulivyosema, anatumia siri zako zote kuwa silaha za kukuangamiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…