Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Waliokuwa marais wa Marekani Barack Obama, George W. Bush na Bill Clinton wamejitolea kupewa chanjo ya ugonjwa wa corona kwa uwazi kabisa.
Watatu hao ambao wawili ni wa chama cha Democrat na mmoja wa Republican wamesema kuwa watapata chanjo hiyo punde tu itakapoidhinishwa na wadhibiti wa maafisa wa afya. Hatua hiyo inakusudiwa kuimarisha imani ya raia juu ya usalama na ufanisi wa chanjo za virusi vya corona.
Kura za maoni zinaonesha kuwa idadi kubwa ya watu hawana haraka ya kupata chanjo hiyo.
Hadi kufikia sasa hakuna chanjo ambayo imeidhinishwa na Marekani lakini wadhibiti wa serikali wanaanza kufuatilia chanjo ya kampuni za kampuni za Pfizer na Moderna wiki zijazo.
"Nawaahidi itakapoanza kupatikana kwa watu walio katika hatari kubwa, nitaipata," Bwana Obama amesema katika mahojiano ya radio Jumatano SiriusXM.
"Huenda nikainywa kupitia televisheni au nichukuliwe video, ili watu wajue kwamba ninaamini sayansi."