beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa Makumbusho ya Marais katika Mji Mkuu wa Taifa letu, Dodoma. Akizungumzia hatua hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana amesema wapo Viongozi wengi walioihudumia Tanzania na Wizara imeona ni wakati mwafaka kuanza ujenzi.
Kwa mujibu wa Waziri Chana, Makumbusho itasaidia kuonesha kwa jamii mchango wa Marais katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa kipindi walichokuwa madarakani.
Swali fikirishi: Wakati kuna changamoto mbalimbali zinazowakumba Wananchi, kuanzia gharama za maisha, utoaji huduma na nyinginezo, ni kweli huu ni wakati "mwafaka" wa Makumbusho?
Kwanini jitihada kubwa sana zinatumika kuonesha "mchango" ilihali ni sehemu ya wajibu wa Viongozi wetu?