Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Kuna kitu nimesikia hivi karibuni kuna watu wanasema 'hatuwezi kujibizana na mgonjwa'. Mimi nimeichukulia kauli hiyo kama tu kucheza na fikra za watu wengi (hasa huku kwetu wengi bado wanawachukulia walemavu kama robo-watu) kuwa mlemavu hajakamilika na kwamba hana uwezo wa kuongoza.
Nimetafakari jinsi maraisi wengi wa nchi kama Marekani wanapopata nafasi ya kuongoza, wanatumia changamoto mbalimbali walizopitia au wanazopitia kubadilisha maisha ya wengine wenye matatizo hayo hayo.
Nikamkumbuka Franklin Delano Roosevelt (maarufu kama FDR), mmoja wa maraisi ambao Wamarekani wanamchukulia ni bora zaidi kutokea nchini kwao na duniani kiujumla. Huyu ni Raisi PEKEE wa Marekani aliyeshinda kwa miula 4 katika historia ya Marekani (na hakufanya hivyo kwa kuchakachua katiba). Kilichofanya nimkumbuke ni kwamba karibu miaka 10 kabla ya kushinda uraisi alipata ugonjwa (kuna wanaosema ni polio) uliomlazimisha kutumia gongo, leg braces na wheelchair. Alitawala kipindi chote cha uraisi (miaka 12) akitumia hivo vitu.
Kwenye biography aliyoandika mke wake, anasema experience hiyo ilimfanya FDR kuyaangalia maisha katika jicho tofauti, kujenga uvumilivu na kutokata tamaa. Zote hizi zilikuwa ni sifa zilizomsaidia sana katika kuongoza.
Ni muhimu nikipoint kuwa kipindi kile wasaidizi wa FDR walijitahidi sana asipigwe picha akiwa kwenye wheelchair. Bado kipindi kile hata wao walikuwa na ‘stigma’ ya uwezo wa mtu mwenye ulemavu.
Ningeomba mtakaosoma uzi huu mgoogle historia nzima ya FDR na utendaji wake kama Raisi na discussion nzima ya ugonjwa wake. Kuna mengi ya kujifunza.