Marais Wastaafu kemeeni uvinjifu wa Katiba, Pia suluhisheni migogoro ya kisiasa nchini kati ya CCM na upinzani

Marais Wastaafu kemeeni uvinjifu wa Katiba, Pia suluhisheni migogoro ya kisiasa nchini kati ya CCM na upinzani

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Binafsi nilifarijika sana uwepo wa Marais Wastaafu Kwani ni TUNU kwa RAIS aliyopo madarakani na wananchi kwa Ujumla.

Binafsi niliamini Marais Wastaafu hao ndio watakuwa mstari wa Mbele kuhakikisha nchi inatawaliwa Kwa mujibu wa Katiba Haki na Sheria zinafuatwa na kama Kuna Utofauti watatumia busara na hekima kumshauri RAIS aliyepo madarakani.

Hivi karibu hasa Katika Utawala wa Hayati Magufuli tumeshuhudia uvunjwaji wa katiba kwa makusudi wa viongozi walioapa kuilinda na Wananchi kuteswa sana.

1. Watu Wamebambikiziwa Kesi

2. Uchaguzi Mkuu Umevurugwa

3. Wabunge 19 wasio na Sifa Wapo Bunge Wanalipwa Mishahara

4 . Vyama vya Siasa Vinazuiwa Kufanya Mikutano Ccm Wanafanya N.k

Mambo ambayo Yanapoteza mshikamano na umoja wetu kwa wananchi .

Binafsi niliamini marais wastaafu ndio mambo Walitakiwa wanamshauri Rais ayaweke Sawa badala ya Rais Kuwasikiliza watendaji wake Ambao ndio chanzo cha yote hayo.

Mbona marais wetu wastaafu wanatumika kusuluhisha migogoro ya kisiasa nje ya nchi kwanini Migogoro ya Tanzania hawajihusishi?
 
Thread zinazofanana ni nyingi mno

Zingeunganishwa tu
 
Tafuta hela kaka tafuta ela. Kama Huna ela kwenye Maisha yako kila mtu utamuona hafanyi majukumu yake ipasavyo
 
Marais wastaafu hawana maana yoyote hao. Wameamua kuweka maslahi yao binafsi na ya maccm mbele na kudharau maslahi ya Tanzania. Niliwahi kuona video ya Kikwete baada ya kurudi toka kusimamia uchaguzi akisifia jinsi Nigeria kulivyo na uwazi wa hali ya juu kwenye kuhesabu kura hadharani huku wanachama na wapenzi wa vyama mbali mbali wakiwepo hapo kushuhudia kwa wingi bila kubughudhiwa na police.

Cha kushangaza sijawahi kumsikia akiitaka hiyo Tume FAKE ya uchaguzi iige utaratibu huo.

Juzi alienda jangwani kwenye mjadala wa Katiba ya yanga lakini cha kushangaza kwenye katiba ya nchi HAHUSIKI kapiga kimya!!!
 
Wazee wanakula per diem kwenye ziara za kutazama miradi ya serikali
 
Hawa wazee wanakula hela ya umma tena kubwa tu kwa mwezi ila hawawasàidii watanzania chochote kudai haki zao za kikatiba zinazoporwa na watawala...kuna faida gani sasa kama taifa kuwa na wazee kama hawa.

CCM inawajaza uwoga hadi hawa wazee maskini ya Mungu kushindwa kukemea maovu nchini.

Yaani tumefikia pahala Rais aliyeko madarakani akisema chocolate kile basi kinageuka kuwa sheria na hawa wazee wapo ila woga umewajaa.

Sasa hivi kuna vuguvugu la katiba ila wapo kimya as if hawapo Tanzania.
 
Daaa!! Is a matter of common sense!!, Mfumo Uliopo Ndio Umewaweka Madarakana na Watoto wao Wanautegemea Kuingia au Kusalia Madarakani. So brother Usitegemee Move Yoyote ya Kuupiga Mfumo uliopo Kuanzishwa na Hao Unaowasema. So If you're serious then, Tuliza kichwa Ungana na Wapinzani plus Activities Kupambana Ili Kupata Unachoamini ni Haki yako.
 
Wastaafu wetu ni waganga njaa hawathubutu kumwambia ukweli rais wasije wskakosa mahekalu na magari ya fahari.
 
Mama Samia ameanza kukosea kwa kuminya demokrasia kama alivyokuwa jp na yeye asipokuwa mwangalifu ataangamia kama mtangulizi wake, mtu yeyote asicheze na haki za watu.
 
Hao Marais wastaafu walifanya nini wakiwa madarakani?
 
Back
Top Bottom