Elections 2010 Marando amgeukia Jaji Mkuu

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
• Amtaka aache kuikingia kifua CCM

Na Mwandishi Wetu, Tanzania Daima

SIKU chache baada ya mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando, kuwahusisha vigogo wa CCM na ukwapuaji wa mabilioni ya fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), amemshukia Jaji Mkuu, Agustino Ramadhan, akimtaka aache kuikingia kifua CCM.

Marando alisema kama Jaji Mkuu Ramadhan anataka kuingia kwenye siasa, ni vema akanunua sare za chama hicho na kupanda jukwaani kujibu hoja na tuhuma zinazoelekezwa kwa vigogo wa CCM wanaohusishwa na vitendo vya ufisadi.

Akizungumza na Tanzania Daima, Marando alisema baadhi ya vyombo vya habari juzi vilimnukuu Jaji Mkuu akiwaonya wanasiasa akiwemo yeye (Marando) kuwa wanaotoa hotuba za kisiasa majukwaani juu ya kesi zilizo mahakamani wanafanya makosa.

Marando alisema anasikitishwa na kauli hiyo kwa kuwa jaji mkuu si mwanasiasa na hapaswi kusikiliza maneno ya kisiasa na kuyatolea ufafanuzi kama hayajafikishwa mezani kwake.

Alisema katika uzinduzi wa kampeni za CHADEMA, yeye (Marando) alisema watuhumiwa waliofikishwa mahakamani kwenye kesi za wizi wa EPA ni matawi tu na kuwataja baadhi ya vigogo wa CCM ambao walipaswa kuunganishwa katika kesi hizo kwa sababu wao ndio walioubariki wizi huo.

Alisema kauli hiyo si kuingilia mwenendo wa kesi bali kuonyesha kuwa kuna mafisadi wengi ambao walistahili kufikishwa mahakamani, lakini hawajafikishwa kwa sababu ya kinga ya chama au wanatumia madaraka yao.

"Jaji Mkuu anatumia kofia yake kuitetea CCM, anataka jamii ione ninachokifanya mimi na CHADEMA ni kosa, hii si sahihi, namuomba aache kubishana na mimi kuhusu masuala ya kisiasa," alisisitiza Marando.

Marando alibainisha kuwa kuna chombo kinachoshughulikia nidhamu ya mawakili hivyo kama yeye atakuwa amefanya makosa chombo hicho kitamuita kumuonya na ikiwezekana kumuadhibu lakini si anavyofanya Jaji Mkuu.

"Yeye kama ana hamu ya kupanda jukwaani si akanunue sare ofisi za CCM pale Lumumba ili tuweze kupambana naye kwenye uwanja unaostahili?" alisema Marando.

Aliongeza kuwa Jaji Mkuu ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, hivyo ana uwanja mpana wa kutolea uamuzi au ufafanuzi kesi inayopelekwa mezani kwake na si maneno yanayosemwa katika viwanja vya Jangwani au vinginevyo katika kampeni zinazoendelea hivi sasa.

Alisema ufisadi ni hoja nzito ambayo haipaswi kupindishwa pindishwa au kutetewa na viongozi kwa sababu imewafanya Watanzania waendelee kuwa maskini katika ardhi yao, huku watu wachache wakitumia rasilimali za nchi kwa maslahi binafsi.

Aliongeza kuwa kutokana na kutambua athari za ufisadi, CHADEMA imeamua kuuvalia njuga na kuwaumbua wale wote walioshiriki au wanaoendelea kutenda vitendo hivyo.

Juzi baadhi ya vyombo vya habari, vilimkariri Jaji Mkuu Ramadhan kuwa kujadili kesi zinazoendeshwa mahakamani kwenye mikutano ya hadhara ni kinyume cha sheria na mahakama itachukua hatua dhidi ya watu wanaofanya hivyo.

Vyombo hivyo vilimkariri Jaji Mkuu akisema kuwa sheria iko wazi kwa wanaoingilia mwenendo wa kesi na mahakama itawawajibisha wanasiasa wanaofanya hivyo bila hata kungoja vyombo vingine vya dola kuwachukulia hatua wahusika.
 
Huyu Jaji Mkuu vipi? inaelekea anatumika sana huyu!! kuna mtu hapa jamvini anaweza kuskumbusha ile kesi ya mgombea binafsi iliisha je? anatumika sana huyu !
 
Tangu lini huyu aliacha ukada wa CCM? Mnasahau huyu alipata kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Muungano (NEC) na pia Makamu Mwenyekiti wa ZEC katika chaguzi 3 -- yaani za 1995, 2000 nq 2005. Katika chaguzi hizo alonyesha u-CCM wake wa hali ya juu hasa mwaka 1995 NEC ilipovurunda uchaguzi kwa mkoa wa Dsm ili kuinufaisha CCM dhidi ya dhoruba la NCCR.

Lakini achilia hii, pia alihusika katika uvurundwaji wa chaguzi zote 3 za Visiwani kwani alikuwa mshiriki mkubwa katika maamuzi ya ZEC katika kuinyima ushindi CUF. Isitoshe baada ya uchaguzi ule wa 2000 kulitokea mauaji makubwa kule Pemba, baada ya wana-CUF kufyatuliwa risasi za moto na polisi, wakati walipokuwa wanaandamana kwa amani kutokana na maamuzi yaki uonezi ya ZEC -- kwani kosa lao lilikuwa kudai tume huru ya uchaguzi. Hatukusikia hata siku moja huyu Jaji Augustine Ramadhani akilaani mauaji hayo au kukomment chochote kuhusu nayo.
 
Yupo kwenye list ya hawa

Lt.Col(Rtd) J.M.Kikwete
Lt.(Rtd)Y.Makamba
Capt(Rtd)J.Chiligati
Brg.Gen(Rtd)A.Ramadhan
.
.
.
and the lsi never end

Failed and non-creered slodiers
 
Me sioni cha ajabu kwa viongozi wetu. Jaji mkuu amepoteza integrity kwa jamii ya TZ tangu alipotoa maamuzi ya kesi ya mgombea binafsi.
 
Huyo inaelekea ameogeshewa maji ya bendera ya CCM ili kote apitapo yeye ni CCM anasahau wajibu wake kama Jaji Mkuu kuwa haruhusiwi kushabikia chama chochote cha siasa hadi atakapo staafu! akiona hawezi vumilia aweke manyaka chini ya Ujaji Mkuu ainge kwenye siasa lakini kama amekalia hicho kiti hapaswi kushabikia Siasa.

Kwenye RED hawezi sema chochote maana angewageuka wangemtuhumu kuwa sio Mtanzania na mengine mengi yangepandikizwa juu yake
 
Huyo ni choka mbaya. Viongozi wengi hawajui kuweka mstari (line of demarcation) na siasa.
 
Anachojua kwa umakini ni kupiga piano pale St.Albans na baadae a warm handshake kutoka kwa Wazee Rupia na Malechela
 
Huyo Jaji mkuu ni mamluki na kada wa chama cha kijana. Anaipeleka nchi kubaya. Hajui misingi ya kazi yake ndo maana anaiendesha kisiasa. Jaji mkuu hatakiwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa,sasa tumweleweje? Anatukumbusha machungu ya mgombea binafsi!
 
Yupo kwenye list ya hawa

Lt.Col(Rtd) J.M.Kikwete
Lt.(Rtd)Y.Makamba
Capt(Rtd)J.Chiligati
Brg.Gen(Rtd)A.Ramadhan
.
.
.
and the lsi never end

Failed and non-creered slodiers

Kaka umelenga penyewe. Nchi inaendeshwa KIJESHI umesahau wakuu wa mikoa na wilaya wengi ambao ni makamanda wa jeshi, viongozi wa CCM nao pia akiwamo Kanali Abdulrahman Kinana, Capten John Chiligati, Kapteni George Mkuchika the list goes hadi ngazi za chini kabisa. Lakini pia huju Jaji yuko katika hatua za kustaafu, usishangae ukasikia zaidi ya hayo kabla na baada ya kustaafu kwake. MUNGU ATATUNUSURU NA KUWAONEA HURUMA WATANZANIA KWA KUENDELEA KUBEBESHWA MATATIZO WAKATI WANYO RASILIMALI NA WATU WA KUTOSHA.
 
kwa hiyo inawezekana naye yupo kwenye mtandao wa J.M.K

Sio inawezekana bali ni mmoja wao ndio maana akapewa Ujaji Mkuu kama fadhila.

Hivyo bado ana mawazo ya kimtandao na kuendelea kuulinda ufisadi
 
Marando amgeukia Jaji Mkuu

• Amtaka aache kuikingia kifua CCM

na Mwandishi wetu

SIKU chache baada ya mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando, kuwahusisha vigogo wa CCM na ukwapuaji wa mabilioni ya fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), amemshukia Jaji Mkuu, Agustino Ramadhan, akimtaka aache kuikingia kifua CCM.

Marando alisema kama Jaji Mkuu Ramadhan anataka kuingia kwenye siasa, ni vema akanunua sare za chama hicho na kupanda jukwaani kujibu hoja na tuhuma zinazoelekezwa kwa vigogo wa CCM wanaohusishwa na vitendo vya ufisadi.

Akizungumza na Tanzania Daima, Marando alisema baadhi ya vyombo vya habari juzi vilimnukuu Jaji Mkuu akiwaonya wanasiasa akiwemo yeye (Marando) kuwa wanaotoa hotuba za kisiasa majukwaani juu ya kesi zilizo mahakamani wanafanya makosa.

Marando alisema anasikitishwa na kauli hiyo kwa kuwa jaji mkuu si mwanasiasa na hapaswi kusikiliza maneno ya kisiasa na kuyatolea ufafanuzi kama hayajafikishwa mezani kwake.

Alisema katika uzinduzi wa kampeni za CHADEMA, yeye (Marando) alisema watuhumiwa waliofikishwa mahakamani kwenye kesi za wizi wa EPA ni matawi tu na kuwataja baadhi ya vigogo wa CCM ambao walipaswa kuunganishwa katika kesi hizo kwa sababu wao ndio walioubariki wizi huo.

Alisema kauli hiyo si kuingilia mwenendo wa kesi bali kuonyesha kuwa kuna mafisadi wengi ambao walistahili kufikishwa mahakamani, lakini hawajafikishwa kwa sababu ya kinga ya chama au wanatumia madaraka yao.

"Jaji Mkuu anatumia kofia yake kuitetea CCM, anataka jamii ione ninachokifanya mimi na CHADEMA ni kosa, hii si sahihi, namuomba aache kubishana na mimi kuhusu masuala ya kisiasa," alisisitiza Marando.

Marando alibainisha kuwa kuna chombo kinachoshughulikia nidhamu ya mawakili hivyo kama yeye atakuwa amefanya makosa chombo hicho kitamuita kumuonya na ikiwezekana kumuadhibu lakini si anavyofanya Jaji Mkuu.

"Yeye kama ana hamu ya kupanda jukwaani si akanunue sare ofisi za CCM pale Lumumba ili tuweze kupambana naye kwenye uwanja unaostahili?" alisema Marando.

Aliongeza kuwa Jaji Mkuu ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, hivyo ana uwanja mpana wa kutolea uamuzi au ufafanuzi kesi inayopelekwa mezani kwake na si maneno yanayosemwa katika viwanja vya Jangwani au vinginevyo katika kampeni zinazoendelea hivi sasa.

Alisema ufisadi ni hoja nzito ambayo haipaswi kupindishwa pindishwa au kutetewa na viongozi kwa sababu imewafanya Watanzania waendelee kuwa maskini katika ardhi yao, huku watu wachache wakitumia rasilimali za nchi kwa maslahi binafsi.

Aliongeza kuwa kutokana na kutambua athari za ufisadi, CHADEMA imeamua kuuvalia njuga na kuwaumbua wale wote walioshiriki au wanaoendelea kutenda vitendo hivyo.

Juzi baadhi ya vyombo vya habari, vilimkariri Jaji Mkuu Ramadhan kuwa kujadili kesi zinazoendeshwa mahakamani kwenye mikutano ya hadhara ni kinyume cha sheria na mahakama itachukua hatua dhidi ya watu wanaofanya hivyo.

Vyombo hivyo vilimkariri Jaji Mkuu akisema kuwa sheria iko wazi kwa wanaoingilia mwenendo wa kesi na mahakama itawawajibisha wanasiasa wanaofanya hivyo bila hata kungoja vyombo vingine vya dola kuwachukulia hatua wahusika.

Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=18975
 
patamu hapo, chuma kimeshika moto nani wa kukikamata kwa mikono? twen zetu Marando!!
 
Hukumu aliyoitoa katika kesi ya mgombea huru, ilimwacha 'uchi' kabisa, alijionyesha wazi kuwa yeye ni gwanda la kijani katika joho la ujaji. Jamii haimwamini tena! Alijipotezea yeye mwenyewe heshima ya jaji kiongozi na hivyo sasa hastahili kukemea wengine.
Isitoshe Marando aliloongea si kesi zilizo mahakamani - aliongelea wale ambao hawajapelekwa mahakamani,
Jaji mkuu kama hata kusikia unasikia kwa 'makengeza'! inasikitisha.
Ulipotoa hukumu ile watu walisema -loo sasa tutakimbilia wapi? Ulipaswa kulijua hilo kabla ya kutoa hukumu. Mahakama ya rufaa tena jopo la majaji walipaswa kusoma mazingira mbalimbali ya kesi ile kabla ya kutoa hukumu au hukujua kuwa hukumu yako ni sheria tayari?
 
Aluta continua............................
 
Hivi mangapi yamekuwa yakizungumzwa na kuandikwa katika magazeti kuhusu kesi mbali mbali zilizopo mahakamani lakini huyu Jaji hakuwahi kukemea. Mfano hai ni ile kesi ya Zombe -- jinsi mambo ya mahakamani yalivyokuwa yanaripootiwa na baadhi ya magazet!!! Ungeweza kusema Zombe angehukumiwa kunyongwa mara kumi!! Sikuwahi kumsikia Jaji huyu akiyakemea hayo magazeti.
 
Ni bora anyamaze kimya kwa huu muda uliobaki,historia itamhukumu.
 
Hivi Serikali ilikata rufaa kupinga hukumu ya Zombe kama walivyokuwa wamenuia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…