Marc Guehi aandika "Yesu Anakupenda" kwenye kitambaa cha unahodha chenye rangi za Upinde, baada ya onyo la FA

Marc Guehi aandika "Yesu Anakupenda" kwenye kitambaa cha unahodha chenye rangi za Upinde, baada ya onyo la FA

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Baada ya kupewa onyo na Shirikisho la Soka (FA) kwa kuandika maneno "I love Jesus" kwenye utepe wa upinde wa mvua, Marc Guehi, beki wa Crystal Palace, ameandika "Jesus loves you" (Yesu anakupenda) kwenye utepe wake wakati wa mechi dhidi ya Ipswich.
IMG_1217.jpeg

Nahodha wa Ipswich, Sam Morsy, naye ameamua kutovaa tena utepe wa upinde wa mvua kutokana na imani zake za kidini.

Soma, Pia:

Guéhi aibua gumzo EPL baada ya kuandika 'I Love Jesus' kwenye kitambaa cha unahodha chenye rangi za upinde/LGBTQ+

Nahodha wa Ipswich Town, Sam Morsy agomea kuvaa kitambaa cha Unahodha chenye Upinde kwa sababu za Kidini

Hatua hizi zimeibua mjadala kuhusu uhuru wa kidini katika michezo, huku wachezaji wakisisitiza haki yao ya kuonyesha imani zao bila vizuizi.
 
Bora waamke wasilazimishwe hayo mavitambaa
 
Ni sawa kwenda msikitini uqndike Yesu ni Mungu au Yesu ni Allah.
Hiyo michezo ni hao mabwana ndio maana wanakuwa wakali ukiwaingizia mambo ya dini kwenye projects zao.
 
Naona Wazungu wamepita kwenye kile kilele cha ustaarabu wa kibinadamu, na sasa wanarudi kuwa kama mahayawani.
Hata wanyama hawafanyi huo upuuzi, ya mbuzi iko wazi sana lakini hata siku moja beberu hakosei akaweka ndipo sipo .
 
Back
Top Bottom