Ndugu yangu kwa upande wangu naona ni vigumu kukupa ushauri au kulinganisha magari tajwa kwa sababu kubwa moja,ni vigumu sana kutoa ulinganisho wa maana kwa magari ambayo yapo makundi tofauti.
Ninachomaanisha makundi tofauti ni kwamba soko lengwa na hayo magari ni tofauti. Hapo magari yaliyo class moja ni mercedes E class and BMW 5 series----family sedan
Mercedes SLK ni coupe/roadster magari yaliyo kundi moja na hilo ni kama Audi TT/BMW Z4 etc etc
Volvo V40 ni hatchback/hothatch na magari ya kundi hilo ni kama bmw hatchback/mercedes A class/Audi A3 etc etc.