March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

By CAPITAL REPORTER | March 4, 2013 (streaming)

1145pm Uhuru 719,798 Raila 510,686


Delayed Uptodate IDC SERVERS ARE DOWN; Some went back to PAPER VOTING it is 2AM March 5th People are still Voting in Kenya

 
Uchaguzi wa kenya umekaa zaidi kikabila haiwezekani sehemu mmoja apate 99% na mwingine 0.5%
 
Jamani naangalia haya matokeo ya uchaguzi wa Kenya, naona kwamba kila mgombea anakotoka anapata zaidi ya asilimia 90. Sasa najiuliza hivi kweli walihitaji kampeni za gharama na nguvu kiasi kile wakati wapiga kura wao walishadecice kwamba kila mtu atamchagua mtu wao?

Hizo ni fikra zangu tu.
 
Hiyo nimekupata bafo ni mchuano mkali na wala huwezi kusema nani ni mshindi kwa sasa....na tusubiri tuone
 
Kuna bookie mmoja alisema uchaguzi ulimalizika Disemba usajili ulipomalizika, kwa sababu ya demographics za ukabila.

Akajibiwa kwamba hakuna kabila lenye watu zaidi ya 22%, kwa hiyo hata kama kila mtu akipigia kiongozi wa kabila lake hakuna atakayefikisha 50%.
 
Teh teh teh hiyo ni kweli Kiranga, lakini alliance zao ziliongeza namba kwenye makabila.

Kiranga usinichukulie serious sana, lakini haya matokeo yalinifanya nijiulize hivi kampeni huwa ni kwa ajili ya kumshawishi nani, yule ambaye ameshafanya maamuzi au yule ambaye bado? It was just a reflection. Inawezekana wale wataalamu wa sayansi ya siasa wanaweza kunisaidia kudadavua zaidi
 
licha ya ukabila wao lakini bado tutampata ambaye wamemchagua kuhusu gharama za kampeni huo ni ugonjwa wa siasa za africa kama uchaguzi wa :crying: udiwani unatumia mabilioni urais inakuwaje lakini tutafika tu
 
Nairobi 48% Raila, 47% Uhuru, this what we can call presidential election results.

ZeMarcopolo na hii unaweza kweli kuiita tight race, siyo hizo sarakasi za kikabila. Ukweli ni kwamba hawa jamaa wamepoteza nafasi kubwa sana ya political leadership in East Africa. Wameweza kutengeneza katiba nzuri, lakini wanaishia kuchaguana kikabila
 

Trust me sijakuchukulia seriously.

Inawezekana hawakuwa na haja za kufanya kampeni sana kwao. Lakini kuna sehemu kama za wa Kalenjin huko kwa kina Moi na Ruto. Wakalenjin wamekuwa swing voters, kwa sababu mtu wao Ruto so one would think wangepiga kura kumpigia Uhuru, kwa sababu running mate wake ni Ruto.

Lakini Wa Kalenjin hao hao wamepigana sana na Wakikuyu, kwa hiyo wanaweza wasimpigie kura Uhuru kwa sababu hiyo. It's not as easy as 123.

Huko kwa waLuo kuna watu wako kama Miguna Miguna kibao, wanaona Raila alivyopata u PM kabweteka, wanataka kummwaga pia.
 

Yeah hiyo ni kweli, lakini ukiangalia intensity ya kampeni na idadi ya swing voters yaani unapata wasiwasi kama kweli kampeni zilistahili nguvu kiasi kile. Lakini kama unavyosema uoga wa kumwagwa pengine uliongezea uzito wa kampeni
 


Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta anaongoza, huku akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Raila Odinga.



Kama alivyo Uhuru, Raila pia ni mtoto wa mmoja wa waasisi wa taifa la Kenya, ambaye alikuwa Makamu wa Mzee Kenyatta, Jaramong Oginga Odinga.

Hadi majira haya ya saa 6.45 usiku wa kuamkia leo, Uhuru ambaye ni mgombea wa TNA alikuwa amepata kura 744,648 sawa na asilimia 56.1 wakati Raila ambaye ni mgombea wa ODM alikuwa akifuatia kwa kupata kura 527, 780 sawa na asilimia 39.7.

Matokeo hayo ni kutoka katika vituo zaidi ya 5000 kati ya 31,000 na yalikuwa yakionyeshwa moja kwa moja na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kadri yalivyokuwa yanaingia.

Hata hivyo Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan akizungumza na vyombo vya habari jana usiku alisema matokeo hayo ni ya awali na kwamba matokeo kamili yangetangazwa na tume yake baada ya kukusanya taarifa kutoka vituo vyote vya kupigia kura.

Wagombea wengine walikuwa wameachwa mbali. Hao ni Musalia Mudavadi, Peter Kenneth, James Kiyiapi, Martha Karua, Mohamed Dida na Paul Muite.

Waliokufa wafikia 22
Wapema watu 22 wakiwamo askari polisi tisa waliripotiwa kuuwawa baada ya kuvamiwa na kikundi cha watu zaidi ya 200 huko Mombasa na Kilifi saa chache kabla ya Wakenya kuanza kupiga kura jana.

Saa chache kabla ya uchaguzi huo, askari polisi tisa waliuawa katika mashambulizi yaliyotokea kwenye miji ya Mombasa, Kilifi na Kwale na kuacha wavamizi wapatao 10 na raia wa kawaida watatu pia wakifariki.

Baada ya vifo hivyo, serikali ilipeleka vikosi vya askari kutoka Mariakani Barracks kwenda kutuliza ghasia hizo wakati kundi lingine la askari lilitoka Nyali Barracks kwa ajili ya kuweka doria katika miji ya Mombasa na North Coast.

Taarifa zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa kwenye mji wa Mombasa askari polisi wanne waliuawa na watu zaidi ya 100 waliovamia kituo cha kura cha Miritini.

Polisi pia ilithibitisha kuuawa kwa watu saba katika mapigano hayo huku na wengine kadhaa kutiwa nguvuni.

Wavamizi wengine waliuawa katika miji ya Kisauni na Kilifi huku polisi wanne wakiuawa Chumani na mmoja huko Chonyi huku watu watatu wakiuawa kwa kupigwa risasi.



Wakati huo huo, mwanamke mmoja wa miaka 72 alianguka na kufariki akiwa kwenye foleni ya kupiga kura katika kituo cha Kaunti ya Murang'a.

Marehemu aliyefahamuika kwa jina la Wanjiku Maina alianguka saa tatu asubuhi katika kituo hicho kilichopo Shule ya Msingi Kaganda katika jimbo la Kiharu na alifariki wakati akikimbizwa Hospitali ya Muriranjas.

Mkuu wa Polisi Kenya, David Kimaiyo alisema Kikundi cha Mombasa Republican Council (MRC), ndicho kinachohusika na shambulio hilo na wafuasi wake wawili wametiwa mbaroni.

"Askari wameelekezwa kutumia silaha kadiri wanavyotakiwa na sheria, ili kuhakikisha hakuna mauaji mengine ya polisi na raia yanatokea," alisema Kimaiyo.

Wajitokeza kwa wingi
Wananchi walijitokeza kwa wingi katika maeneo mbalimbali jana kupiga kura.

Wakati vituo vilikuwa vinafunguliwa saa 12 asubuhi, watu walianza kufurika vituoni saa 8.00 na saa 9.00 usiku ili kuwahi nafasi na ilipofika muda uliopangwa, misururu ilikuwa mirefu kupindukia.

Katika vituo, ambavyo Mwananchi ilitembelea, pamoja na wingi wa watu, bado wapigakura walikuwa na matumaini ya kuchagua viongozi wao.

Hata hivyo, kulikuwa na matukio kadhaa ya kukatisha tamaa, ikiwamo kukwama kwa mashine za digitali za kutambua alama za vidole za waliojiandikisha (biometric machines).

Baadhi ya mashine, ziliathiriwa na hitilafu wakati nyingine zikikosa umeme katika vituo vingi vya maeneo mbalimbali ya Kenya, hivyo makarani kulazimika kutumia daftari la wapigakura.

Mwenyekiti wa IEBC, Hassan alikiri kuwapo kwa hali hiyo na kusema ingetafutiwa ufumbuzi na kuahidi kuwa muda ambao ungepotea ungefidiwa baadaye jioni.

Katika hatua nyingine; watu wawili akiwamo mwanamke mwenye umri wa miaka 72, walianguka na kufariki dunia wakati wakisubiri kupiga kura.

Mwanamke huyo alipoteza maisha saa 5.08 asubuhi katika Kituo cha Kihalu kwenye Shule ya Msingi Kaganda, Kaunti ya Muranga. Mpigakura mwingine alianguka saa nne asubuhi katika Kituo cha St Mathew, eneo la Hardy, Nairobi. Alifariki akiwa hospitalini.

Kura Arusha, Dar
Mamia ya wananchi wa Kenya wanaoishi Tanzania walipiga kura katika majiji ya Dar es Salaam na Arus



Wakenya hao walipata fursa kwa mujibu wa Katiba Mpya ya nchi hiyo iliyoanza kufanya kazi mwaka 2010.

Ofisa wa IEBC, David Maina ambaye alikuwa anasimamia upigaji huo Arusha, alisema kwamba hadi kufikia saa tisa alasiri jana watu 145 kati ya 200 waliojiandikisha, walipiga kura.


source: Mwananchi gazeti
 
Yeah hiyo ni kweli, lakini ukiangalia intensity ya kampeni na idadi ya swing voters yaani unapata wasiwasi kama kweli kampeni zilistahili nguvu kiasi kile. Lakini kama unavyosema uoga wa kumwagwa pengine uliongezea uzito wa kampeni

Hakuna kitu kibaya kama ukafanya kampeni halafu ukashindwa kwa 1% kwa sababu ulizembea kitu kidogo tu.

Ndicho walichokuwa wanataka kuepuka naona.

Ukiweka msuli wote, hata ukishindwa unajua umeshindwa baada ya effort yote.

Ukizembea hwishi kujilaumu baadaye.
 
Saver ya matokeo haifanyi kazi. Tatizo la wakenya wamejifanya kwenda electronic wakati hakuna umeme wa kutosha. Battery hazichargiwa na zoezi lishachauka tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…