Nilianza kuona kazi za Marco Tibasima kwenye Msanii Afrika la Sahara Communications (RFA, Star TV) wakati huo likiwa ni Jarida Kabisa na si gazeti. Alikuwa na mwenzake Oscar Makoye (Tolu). Baadaye akahamia jarida la Ambha la Amri Mbwana Makata Bhawji. Baadaye Sani. Baadaye akapotea... sijui kaenda wapi?!!
NB.
Amri Mbwana Makata Bhawji (nadhani jina Ambha limetokana na Majina yake) ni mdogo wa aliyekuwa mwandishi wa riwaya za Sani Said Mbwana Makata Bhawji. Saidi ndiye mwandishi wa hadithi murua ya Sani iliyoitwa "Maji Mazito" ikiwa na characters akina Omar Kisila (Ommy Kiss), Vicky, Kapuko wa Kapuko a.ka. Maji Mazito. Hakuna wakati ambapo Sani (Jarida) lilikuwa na nguvu kama wakati wa Said Bhawji. Kipindi hicho John Mathias Kaduma (aka Fogasta, aka John Black aka Baba Jack, aka Mmachinga (Moh'd Hussein) "Samba Msele" alikuwa mchoraji mkuu wa Sani. Binafsi sijaona mchoraji aliyekuwa mahiri, nguli na mweledi kama John Kaduma. Never ever. Never. Kaduma ameinfluence sana uchoraji unaoendelea Tanzania kwa sasa. Kuna katuni nikiziona nagundua zimeiba idea fulani ya Kaduma au mchoro wake wa zamani. Mfano "Visa vya Baba Ubaya" anavyochora Issa Lupembe (Dr. Levy) ni initiative ya Kaduma wakati huio akichorea jarida la Kiu kabla ya kufanywa kuwa gazeti la kawaida. Kama sijakosea Kaduma ndiye aliyekuwa anachora kijitabu cha "Visa vya Panga la Shaba." Those Days!!