bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Wale wahenga wa mpira wa miguu lazima watakua wanamjua huyu fundi wa mpira wa miguu mzaliwa wa Brazil mwenye Uraia na Hispania na pia Akichezea timu ya taifa ya Hispania ila michezo michache akianza na mingi akiishia kukaa benchi
Senna Alikua kiungo aliyekamilika akiwa na uwezo mkubwa na kupiga pasi ndefu na zenye uhakika na pia fundi wa kupiga penalti,Muda mwingi ametumia kuchezea klabu chake cha Villarreal cha Hispania
Kiungo huyu fundi Senna alikosa nafasi timu ya taifa na kushindwa kuwika kutokana na timu ya taifa ya Hispania kuwa na wakali wengine Kama vile Xavi ambaye yupo Falme za kiarabu akimalizia mpira wake kwa kula pensheni ya Mwarabu kutokana na Pesa zake za Mafuta na Iniesta yeye akiwa bado yupo Hispania na klabu yake ya Barcelona ambayo ipo uwanjani leo ikicheza na Girona na wakiwa wanaongoza goli 1 huku nikimwona jirani yetu Olunga ndani ya uzi wa Girona.
Marcos Senna ulitupa wapenzi wa mpira vitu adimu nikutakie maisha marefu ukiwa tiyari umetundika daluga.