Marcos Senna Kiungo fundi aliyefichwa na kivuli cha Xavi na Iniesta.

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Wale wahenga wa mpira wa miguu lazima watakua wanamjua huyu fundi wa mpira wa miguu mzaliwa wa Brazil mwenye Uraia na Hispania na pia Akichezea timu ya taifa ya Hispania ila michezo michache akianza na mingi akiishia kukaa benchi

Senna Alikua kiungo aliyekamilika akiwa na uwezo mkubwa na kupiga pasi ndefu na zenye uhakika na pia fundi wa kupiga penalti,Muda mwingi ametumia kuchezea klabu chake cha Villarreal cha Hispania

Kiungo huyu fundi Senna alikosa nafasi timu ya taifa na kushindwa kuwika kutokana na timu ya taifa ya Hispania kuwa na wakali wengine Kama vile Xavi ambaye yupo Falme za kiarabu akimalizia mpira wake kwa kula pensheni ya Mwarabu kutokana na Pesa zake za Mafuta na Iniesta yeye akiwa bado yupo Hispania na klabu yake ya Barcelona ambayo ipo uwanjani leo ikicheza na Girona na wakiwa wanaongoza goli 1 huku nikimwona jirani yetu Olunga ndani ya uzi wa Girona.

Marcos Senna ulitupa wapenzi wa mpira vitu adimu nikutakie maisha marefu ukiwa tiyari umetundika daluga.
 
Mkuu wa Nyambizi ya Villareal,Senna alikuwa ni balaa level zake ni sawa na Pirlo ,Juninho Pernabucano na Rivardo
 
Senna hakufichwa na xavi na iniesta kama ulivyosema bali alikimbizwa na Sergio Busquets katika uero 2008 senna alikuwa muhimili mkubwa wa spain mpaka wanachukua kombe alicheza karibuni mechi zote akianza kuachwa kuitwa national team mara baada ya Pep Guardiola kumvumbua Sergio B.
Na hapo akamfukuzisha yaya toure ktk klabu na marco senna national team kuanzia world cup 2010 alicheza sergio na mpaka leo bado analimiliki dimba la chini pale La Roja
ila yote kwa yote senna alikuwa jembe mtu hatari alivyokuwa ktk ubora wake
 
Mkuu wa Nyambizi ya Villareal,Senna alikuwa ni balaa level zake ni sawa na Pirlo ,Juninho Pernabucano na Rivardo
Itafika mahali hatutaangalia mpira tena mafundi wote wa mpira umri unawatupa wote uliowataja hapo juu akina Pavel Nedved zamani unaangalia mpira mpaka raha sio siku hizi ladha ya soka imepotea kabisa wapo wapi ac Milan ya kaka,Juventus ya David Tzeguet,Inter Milan ya Christian Vieri
 
Ila heshima anayopewa Xavi au Iniesta leo ni tofauti kabisa ya Heshima iliyopewa Marcos Senna zama zake
 
Euro 2008 alikinukisha balaa. Mzee wangu alikuwa ananiambia ubaguzi wa rangi pia ulichangia huyo jamaa kutopata namba spain. Kwa wakati ule nadhani mchezaji mweusi kwenye timu alikuwa peke yake.
 
Hahaaa Zambrotta,Maldini,kiungo mtukutu Gartuso,
 
Ila heshima anayopewa Xavi au Iniesta leo ni tofauti kabisa ya Heshima iliyopewa Marcos Senna zama zake
Aliwika kipindi kifupi sana aling'aa ktk tournament moja tu uero 2008 tofauti na hao viumbe walianza naye uero 2008, world cup 2010 na uero 2012 sasa hapo lazma kutakuwa na utofauti japokuwa alikuwa hatari pia
 
Aliwika kipindi kifupi sana aling'aa ktk tournament moja tu uero 2008 tofauti na hao viumbe walianza naye uero 2008, world cup 2010 na uero 2012 sasa hapo lazma kutakuwa na utofauti japokuwa alikuwa hatari pia
Senna alikuwa Mbrazil alipewa uraia wa Spain mwaka 2006 wakati huo tayari alikuwa na umri mkubwa
 
Mpira wa zamani ulikuwa unanoga ile mbaya watu km lumbergh, ,henry, denis bekhamp, robert pires mtu km rivaldo na dinho mwenye soka lake bila kusahau jay jay okocha mchezaji pekee kuwah kumuona africa aliyekuwa anawavisha madali wazungu
 
Ishu kubwa ni kuwa Marco Senna alivuma wakati umri wake ulikuwa ushasagoea mbele.

Aling'aa katika michuano ya Euro 2008 akiwa na Spain.

Pia kikosini Villareal, alikuwa ndio captain huku akiwa na nyota kama akina Juan Pablo Sorin, Juan Roman Riquelme hakika nyambizi ya Manjano ilitikisa sana.

Kwangu mimi Marco Senna ni miongoni mwa viungo bora wa ulinzi kuwahi kucheza soka kando ya akina Claude Makelele na Xabi Alonso.
 
nimemkumba sanifu lazaro tingisha duu anakimbia goli hadi goli tingisha tingisha goli@tingisha tingisha goli tingisha hatari
 
Hahaaa Zambrotta,Maldini,kiungo mtukutu Gartuso,
Zama zinabadilika na umri ndio umewaondoa ila hata sasa wapo baadhi ya mafundi ila sema mpira umetawaliwa zaidi na promo na media so vipaji halisi vimeachwa tu mtaani ndio maana ukienda kwenye viwanja vya kawaida vya mtaani kuna mpira mkubwa sana unapigwa na vijana wa mtaa
 
Balaa lake halikuwa dogo nakumbuka Euro 2008 ilikuwa n Germany vs Spain ofcoz hyo game Marcos senna alitakata
 
Kuna game moja ya ucl dhidi ya arsenal sijui jamaa alikuwa na jipu kunako. Shughuli ilikuwa Kali kiasi lile jipu lilipasuka bila jamaa kujua. Tulichokuja kushuhudia ni bukta tu imeloa damu afu jamaa anakinukisha tu bila kujali
 
umemaliza kila kitu hapo mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…