Marcus Rashford, kipaji kingine kinachoelekea kufuata nyayo za Adnan Januzaj

Marcus Rashford, kipaji kingine kinachoelekea kufuata nyayo za Adnan Januzaj

Joined
Oct 16, 2015
Posts
20
Reaction score
56
MARCUS RASHFORD
47A57C02-4BDE-4E42-B0AA-FF677C91EC95.jpeg
, KIPAJI KINGINE KINACHOELEKEA KUFUATA NYAYO ZA ADNAN JANUZAJ .

Kalamu ya Nasri Kulemba

Ni usiku wa maajabu ,ni siku nyingine ya ulimwengu kushanga !!! ilikua ni siku ya wanakandanda duniani kushuhudia kipaji kipya kikifanya maajabu ndani ya stadium of light . mashabiki 49,000 wakishuhudia Adnan Januzaj akipiga bao mbili na kuifanya Manchester unites itoke nyuma kwa kutimiza ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watukutu Sunderland .

Ni siku njema kwake Januzaj ..ni siku ambayo daima imebaki ya kepekee kwake,kijana wa umri wa miaka 17 alitambulika rasmi duniani. hama hakika ulikua ni msimu bora kwake chini ya kocha David moyes .

Januzaj ni jina lilotabiliwa makubwa kwenye viunga vya old trafford ,alitabiliwa kuwa ni mrithi wa Ryan Giggs ,alitabiliwa kuwa ni cristiano Ronaldo mpya,Man utd hawakusita kuumpa mkataba wa miaka 5 kwasababu waliona kipaji chake .

Adnan alikua ni kipaji kweli kweli ,alikua na kasi ,mbinu za kupiga chenga na zaidi alikua ni mtulivu na aliweza kujiamini ipasavyo,chini ya Moyes adnan januzaj alikua ni mchezaji tegemeo mbele ya mastaa kama Michael Carrick ,Juan Mata ,patrice Evra na Robin van Persie .

Alijenga mategemeo makubwa ya kuwa mbeleni atakua mchezaji mkubwa na tegemeo pale matofarini … Kiukweli alikua staa ndani ya muda mfupi ,na ndio maana Bbc hakusita kumpa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa msimu .

Lakini ghafla adnan alianza kubadilika ,alikua si yule aliyetabiliwa makubwa ,hakuonesha kuwa ni mtuu mwenye tamaa ya mafanikio ,alipoteza sifa ya kujiamini na ule uwezo wa kupangu ngome ya timu pinzani ulikosekana …

Mwaka 2017 Man United chini ya mkufunzi Josse Mourinho alibaliki juu ya uuzwaji wa Adnan Januzaj ,na Adnan akaelekea Real Sociedad kwa ada ya £ 9.8 million . Na huu ndio ulikua mwisho wa Adnan pale Old trafford ,na ndio ulikua mwisho wa ndoto njema kutoka kwa mashabiki ..

Nini kilichofuata kutoka kwa Adnan …!!nadhani imebakia kuwa ni histori,tumebaki njia panda ,nini kilitokea kwake juu ya umahili wake uwanjani ..ni swali gumu sana linabakia juu ya kichwa chake,labda yeye anamajibu zaidi .

Baada ya miaka miwili ya maajabu na sintofahamu nyingi kutoka kwa Adnani Januzaj,aliondoka Old trafford na kujiunga wa Burrusia Dortmond kwa mkopo wa muda ,ndipo kikaibuka kipaji kingine chini ya mkufunzi Lous Van Gal ,huyu si mwingine ni Marcus Rashford .

Rashford alifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza ya kikosi cha kwanza dhidi ya Midtjylland kwenye UEFA Europa League Februari 2016 na mechi yake ya kwanza ya Premier League dhidi ya Arsenal siku tatu baadaye. Pia alifunga katika mechi yake ya kwanza ya Manchester derby, na pia kwenye mechi yake ya kwanza ya Kombe la EFL na UEFA Champions League. Akiwa na United .

Bahati ilioje..anatoka Adnan anaingia Marcus tena kwa nyakati zinazofuatana ,kipaji cha adnan kilikua kama mfano wa mtu aliyekata muwa na kuanza kuula kisha akawahi kukutana na fundo ,kupita Rashford watu walisahau fundo la kwanza kisha wakautana na ule utamu katika fundo la pili .

Makubwa aliyoyafanya Rashford katika msimu wa 2016/2017 united walikua na kila sababu ya kumsahau kijana wao pendwa na kusahau kila kitu kuhusu yeye katika yale matarajio ,ndipo walioopata nguvu ya kumuuuza akiwa na umri wa miaka 22 .

Impita miaka 5 toka Adnan aondoke na kijiti amuachie Rashford ,mambo mengi yamepita kwa Rashford ; kiwango chake kimekua cha kupanda na kushuka kila msimu ..amekua hana muendelezo bora .

yaliomkuta Adnan ndio yanaomkuta Rashford ,taratibu amenza kupoteza kujiamini ,ule uwezo wa kupiga chenga umepotea,amebakiwa na kasi ya kukimbia uwanjani. lakini anakimbia pasina mipango na uelekeo .

Amekua mvivu na zaidi anaonekana kukata tamaa akiwa kijana kabisa ,tuna ndoto kupitia Rashford ..lakini tunakatishwa tamaa na yeye,haionekani ni lini Rashford atakuja kuwa yule wa ndoto yetu .

Mara kadhaa kipindi cha Josse Mourinho alitamani kumtoa kwa mkopo,lakini bodi na mashabiki hawakukubaliana na jambo hilo ,kwanini ..!! ni kwasababu mashabiki walikua na imani nae ,hawakutaka kuona mwisho wa Marcus mapema ,kama walivyoshuhudia mwisho wa kijana wao Adnan akiwa kinda .

Hawakuamini katika kushindwa Marcus na waliamini katika udhaifu wa mbinu za Josee Mourinho . bahati nzuri muda ndio hakimu kila kitu …muda unazidi kutupa majibu kwa Rashford sio muda mrefu anafuata nyao za jamaa yake Adnan .

Labda itokeee … lakini macho muda mwingine hutupa majibu kutokana na kile tunachokiona hata bila kuwa na mizani .. mwisho wa marcus kwenye kumsubilia unaelekea kufika tamati .

Hasa kwa kiwango chake alichokionesha katika msimu ulioisha ,binafsi naamni msimu mpya kwake Rashford utakua msimu wa majibu kutoka upande wake . kwetu wadau wa soka tumeshapata majibu na ndoto yetu juu yake imeshakatika . sidhani kama kuna shabiki yeyote duniani anategemea maajabu kutoka kwa Marcus .

imebakia juu yake …aturudishe kule katika hisia za imani yetu dhidi yake ama aendelee kutubakisha katika hisia hizi hizi tulizonazo .. la sivyo ataondoka Old trafford kama alivyoondoka swahiba wake huku tukiwa hatujawapata matunda ya faida juu yao .

Instagram Nasrikulemba
au instagram NSK michezo follow .
 
Huyo alikuzwa mno, kifo chake kilianza taratibu baada ya usajili wa Bruno.

Bruno akapewa nafasi ya kupiga mipira ya kutenga pamoja na kupiga penati kitu ambacho kilipunguza nafasi ya Rashidi kufunga. Haikuishia hapo, aliposajiliwa CR7, ndo mambo yakaharibika mazma.
Watu wakawa wanawaza maajabu ya CR7 huku Rashidi akiwa busy na masuala ya kusaidia jamii badala ya kupambana uwanjani.

Mwisho wa siku Rashidi amekosa utulivu, nje ya uwanja msukumo kwa mashabiki wa kutaka magoli toka kwake umemlemea mara dufu. Ameanza maneno ya taarabu kwenye mitandao ya kijamii kupashana na washabaki.

N:B, Wachezaji wengi wa kiingereza huwa wanapotea mapema maana wanaanza kubebeshwa majukumu makubwa wakiwa wadogo, labda itokee mchezaji apate umaarufu akiwa kwenye 20's kidogo huwa wanadumu kwenye mafanikio muda mrefu.


"Kwa ufupi zama za Rashidi zimefika kikomo labda aje kwa Mwamposa kupata mafuta ya upako."
 
Back
Top Bottom