Marefa na Yanga kulikoni mwaka huu?

mpiga vichwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
2,376
Reaction score
3,811
Miaka minne mfululizo ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom ulielekea katika viunga vya mitaa ya msimbazi.

Kwa kipindi chote hicho Tumekuwa tukisikia malalamiko ya kila aina kutoka upande wa pili kwa watani zao Yanga kuwa simba inapendelewa na tff na Marefa hali iliyopelekea mtifuano mkubwa Kati ya tff na Yanga hadi kufikia Mashabiki wa Yanga kuibatiza tff jina tifua tifua na wale wa simba kuwaita Yanga Malalamiko fc.

Msimu huu tangu uanze kwa udhamini wa NBC na baadae mdhamini mwenza GSM hayo malalamiko hayapo tena badala yake marefa na tff ni kusifiwa kila kona na Mashabiki wa timu iliyokuwa mstari wa mbele katika ukosowaji .

Maswali ya kujiuliza ;
1.Je, mwaka huu marefa walipata mafunzo ya kutosha namna ya uchezeshaji hivyo wanazingatia sheria zote 17 za mpira wa miguu na upande huo unaridhika Sana na uwezo wa marefa? Au

2.Yanga walikuwa wanafahamu ukweli wa kikosi chao kwamba ni kibovu ila tff na marefa walikuwa wanaangushiwa tu jumba bovu?Au

3.Kwakuwa GSM ni miongoni mwa wadhamini wa ligi hiyo na vilevile ndiye mdhamini wao, ndiyo Maana Yanga hawalalamiki Maana wanajua miongoni mwa wagawa mkate baba naye yumo?

Nawasilisha. Majibu tafadhari.
Povu rukhusa .
 
Yanga siku zote ndio inanufaika na maamuzi ya refa kama penati ya kisinda, goli kona hata maamuzi mabovu ya namungo mpaka leo refa hajaadhibiwa
 
Yanga siku zote ndio inanufaika na maamuzi ya refa kama penati ya kisinda, goli kona hata maamuzi mabovu ya namungo mpaka leo refa hajaadhibiwa
Penati ya kisinda inatofauti gani na ya Yondani vs Kagere?
Mbona marefa hao hao wakifanya maamuzi ya kuionea Yanga hamzungumzii? Penati ya Saidoo aliyochezewa faulo kwenye mechi na Prisons hamkuiona? Goli la makambo jana lililokataliwa hamkuliona?
 
Yanga waliokuwa wanalalamika kwenye ukweli.. na hata sasa Kama Kuna mtu au taasisi yoyote itaamua kuikandamiza Yanga haitashindwa kulalamika au kulaani makandamizo hayo..

Yanga hoyeeeeeeeee..
Mwaka huu kikombe ni chetu, tulisema tunatangaza ubingwa baada ya mechi 25 tu na sasa zimebaki mechi 15 tu tutangaze ubingwa
 
Penati ya kisinda inatofauti gani na ya Yondani vs Kagere?
Mbona marefa hao hao wakifanya maamuzi ya kuionea Yanga hamzungumzii? Penati ya Saidoo aliyochezewa faulo kwenye mechi na Prisons hamkuiona? Goli la makambo jana lililokataliwa hamkuliona?
Mkuu kubishana na watu ambao kiongozi wao wa juu kabisa kwenye klabu yao aliwaona ni weupe vichwani paka akawabatiza jina la mbumbumbu ni kupoteza muda wako bule
 
Daah akili za Wana utopolo Ni za kutilia mashaka Sana.
Yaan utangaze ubingwa kwa mechi 25 wakati unapumuliwa kisogoni na mnyama !!!
Kwanza uto saiz anashinda kwa mbinde Sana hizo mechi 25 Simba na Azamu watakua wamepoteza michezo 5 kila mmoja huku yanga akiwa hajapoteza hata mmoja ,vipi akil yako inakuambia Hilo linawezekana?
Acha nicheke tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Yanga imechukua ubingwa gizani mara nyingi sana kwa msaada wa waamuzi.
Pamoja na mslalamiko yao mengi miaka minne iliyopita bado wao ndio walifaidika zaidi na makosa ya waamuzi.

Ukweli walizoea kuishi na kikosi cha kawaida ila ushindi wa michongo.Hii inathibitishwa na yanga kutokuwa na historia nzuri kimataifa.

Jambo hili huwezi kuwasikia wachambuzi wa mchongo wakilisema.Kimkakati wachambuzi wengi wanalipwa sasa hivi na GSM ndio maana hawaoni udhaifu wa waamuzi ingawa upo sana
 
Kwahiyo mwaka huu marefa wako vizuri ? Au ni kwakuwa tu bado Yanga haijapoteza mchezo ndo Maana hawalalamiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…