Marefa wa Tanzania wanangoja nini kugomea kuchezesha mechi zote za NBC?

sergio 5

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2017
Posts
9,869
Reaction score
11,484
Hili suala Lilianza toka mwaka jana kwenye DERBY wanaletwa marefa WA kigeni je waamuzi wetu hawaoni kuwa kama kwao Hilo ni tusi kubwa sana

Maana najua wanalipwa pesa kidogo hao waamuzi kutoka nje wanakuja kuchota pesa kibao ata mara 50 ya wanacholipwa wa kwetu

Kwa kulinda heshima zao nawashauri wagomee KUCHEZESHA match za NBC Hadi pale watapo aminiwa na kuheshimiwa
 
Kama unafutailia mpira wa Tz, sababu za kuleta marefa wa nje ni za msingi sana.

1. Ushahidi wa rushwa upo, bahati mbaya tu mamlaka zinakwepa kuchukua hatua kwenye chanzo-timu
2. Hata marefa ni mashabiki wa Simba/Yanga
3. Presha za mashabiki na mpira wenyewe. Ingekuwa refa wa Tz asingetoa ile penati kuogopa lawama
 
Kama ni ivyo huoni mamlaka zina shida Sana ?

Unakubali haki itendeke match moja tu?
 
Tukimalizana na ujingaujinga wa marefa kituo cha pili ni kuleta wazungu waje kuongoza sirikale ya JMT.Belive it or don't!
 
Wagome tu, yule refa aliyechezesha derby taaluma yaje ni mhandisi wa majengo hana njaa kama Kayoko au Aragija.
Hatuwezi kulipa mpira ambao matokeo yanaamriwa na marefa au bingwa anapatikana sababu ya makosa ya marefa.
Halafu kwanini usiwashauri wagome kwa sababu hawaitwi kwenye mechi kubwa za Afrika ambako kuna mpunga mrefu zaidi.
 
Kwaiyo haki iwe inapatikana kwenye match moja tu sio?
 
Arajiga acha njaa
Arajiga ni kocha mzuri kulinganisha na makocha wengine wa bongo sema ni vile mpira wa bongo Kuna siasa nyingi unaweza kukuta kachezesha vizuri ila kosa moja tu likatokea anaonekana ni mbaya kwa mashabiki walioona Hilo kosa halijawanufaisha wao.
 
Arajiga unamuonea tu ni refa mzuri na ni top na anabeg ya Caf sema Kuna baadhi ya mechi unakuta Kuna kosa limetokea Tena la kibinadamu ndio mnalitumia kumuona afai wakati mechi nyingi tu kachezesha vizuri.
 
Arajiga umenyang'anywa tonge mdomoni umeamua kujianzishia uzi ili upate watetezi🤣🤣.. Achana na hizi mechi, mashabiki wa Simba wameshakuonya, watakushushia kimzigo uvae msuli🤣😎
 
Arajiga unamuonea tu ni refa mzuri na ni top na anabeg ya Caf sema Kuna baadhi ya mechi unakuta Kuna kosa limetokea Tena la kibinadamu ndio mnalitumia kumuona afai wakati mechi nyingi tu kachezesha vizuri.
Makosa ganibya kibinadamu yanatendeka mbwlw yake, kama hizi kamati zingekuwa zinafanya kazi kwa haki angekuwa anachezesha daraja la tatu.
 
Hela ya kuendeshea maisha yao atakuwa anawapa mumeo??? Jibu bibie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…