Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Utapeli huu wa Wanaijeria ni maarufu sana; wanakutumia Email. kuingia nawe mikataba ya mabilion ya pesa mnajaziana documents kadhaa na we unawatumia mnaenda sambamba huku ukiwatumia some amount kama 'kishika uchumba', na kukufungulia acccount bank yao huko pamoja na kulipia lipia mambo kadhaa wa kadhaa. Halafu wanakwambia sasa subiria mzigo utumwe.
Kipindi hicho unakuwa busy sana kwenye internet cafe (miaka hiyo) au kwenye computer yako home, basi unaanza kutuulizia kati ya Range Rover na Mercedes Benz au Jeep lipi ni gari zuri. Au kununua nyumba Mbezi Beach, Mikocheni n.k gharama yake ni Tsh ngapi. Unaanza kutafuta madalali na kutuambia TUTAELEWANA TU.
Huu utapeli ni wa miaka mingi sana toka 2000s wala si mpya sema wengi hawaelewi na wamepigwa sana. Hasa madaktari, wanasheria na mainjinia. Na baadhi ya walimu pia. Wanapigwa sana pesa. Najiuliza mzee wa watu alipigwa Tsh ngapi?