Kibo Marealle amekufa usingizini,s iku ya Jumamosi usiku, usiku wa Pasaka, amekufa wakati ule ule ambao Yesu Kristu alipokuwa anafufuka.
Kwa kufa namna hiyo siku ya Pasaka, ina maana kwamba kifo chake miaka yote kitahusishwa katika mawazo yetu na Pasaka.
Kwa wale wanaouliza Kibo ni nani, Marealle yupi, Kibo alikuwa Mweka Hazina wa Shirikisho la Wenye Viwanda vya Kutengeneza Madawa Tanzania, pia Mwenyeketi ya Bodi ya Kampuni ya Madawa aliyoianzisha inaitwa 1997 Pharmaceuticals [nadhani].
Kibo alikuwa 'a nice fellow, always smiling' although I must say in death, he looked very stern, a very serious expression on his face.
Amekufa usingizini, no foul play is suspected, wamekwenda tu kumwamsha asubuhi, wakaona kwamba haamki.
Walisoma wasifu wake katika mazishi, kwamba Kibo alikuwa mkarimu sana. I can testify to that. Last time nilipomwona Kibo, nilimuomba na alinipa, 1000tsh.[it was all I had asked for].
I packed my bags to go to his funeral. Unfortunately nilipofika pale nyumbani kwake, Jangwani Beach, nilichelewa usafiri. Na wale niliowakuta pale walikuwa hawanifahamu, [na mimi pia nilkuwa siwafahamu, isipokuwa tu yule mke wake, Mercy, ambaye nilimuona mara moja tu, siku moja Kibo aliponipeleka nyumbani kwake] they did not notice my presence, they did not acknowledge my presence, they put the casket into the hearse car, they got into their cars and they rode off to Moshi.
Basi, nikaondoka pale. I thought for a moment, nikaamua, I will go to Ubungo to take a bus. Kuhusu wale watu ambao hawakuniona, I will not worry about them, kwa sababu Kibo namfahamu toka zamani.
Kwa hiyo nikaenda Moshi, I attended funeral. Mr. Reginald Mengi pia alihudhuria, [yule mkubwa wa Familia ya Mareallle aliongea maneno mengi kumsifu Mr. Mengi, kwamba, ''wewe Mengi, unafanya Mengi ambayo yanawasaidia wengi.''
Pia alikuwepo Freeman Mbowe na Mama Nsilo Swai, ambaye alikuwa Godmother wa Kibo. Mama Nsilo Swai, alituambia kwamba Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri alituma salamu kwa Familia ya Marealle, na kwamba, apparently, hata Chama Cha Mapinduzi pia kimetuma salamu za rambi rambi. Kwa hiyo nina hakika, Familia ya Marealle ilifarijika.
Pia walikuwepo katika mazishi,Simba Marealle na Janet Marealle,ndugu zake Kibo, baba mmoja, mama mbali mbali.