- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Milton Lupa amefariki juzi kwa ajali ya gari Morogoro. Leo anasomeka mkeka wa uteuzi
How comes? Hivi Katibu Mkuu Kiongozi umeruhusuje huu mkeka kutoka na makosa haya?
CPA Milton Mailos Lupa
How comes? Hivi Katibu Mkuu Kiongozi umeruhusuje huu mkeka kutoka na makosa haya?
CPA Milton Mailos Lupa
- Tunachokijua
- Katika kuboresha utendaji kazi Serikalini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Juni 6, 2024 alifanya uteuzi na uhamisho wa viongozi kadhaa.
Uteuzi huu ulihusisha Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Naibu Makatibu Wakuu, uteuzi na uhamisho wa wakuu wa Wilaya, Uhamisho wa Makatibu tawala wa wilaya, uteuzi na uhamisho wa wakurugenzi watendaji wa Halmashauri pamoja na Uteuzi wa Majaji wa Mahakama kuu kama inavyoonekana hapa.
Baada ya kutolewa kwa taarifa hii, yaliibuka madai mengi mtandaoni yakibainisha kuwa mmojawapo wa wateule kwenye nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Milton Mailos Lupa ni marehemu, hivyo hakupaswa kuwepo kwenye uteuzi huo.
Ukweli wa madai haya
JamiiCheck imefuatilia madai haya na kubaini yana ukweli. Taarifa ya Ikulu iliyochapishwa Mtandaoni kwa mara ya kwanza ambayo JamiiCheck imeihifadhi hapa, jina la 5 kwenye orodha ya Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri lilikuwa la Milton Mailos Lupa.
Hata hivyo, taarifa hiyo iliondolewa baadae na kuchapishwa nyingine ikiwa na mabadiliko yaliyohusisha kuondolewa kwa jina hilo. Taarifa mpya ipo hapa.
Taarifa ya kwanza yenye Jina la Milton Lupa
Kwenye taarifa hii mpya, jina la 5 kwenye orodha ni Upendo Erick Mangali aliyehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Kifo cha Milton Lupa
Baada ya kuhakiki uwepo wa Jina lake kwenye uteuzi, JamiiCheck ilifuatilia pia na kubaini kuwa Milton Mailos Lupa alifariki Juni 4, 2024 kwa ajali ya gari Maeneo ya Dumila, Morogoro akiwa mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA). Taarifa ya kifo hicho imehifadhiwa hapa.
Aidha, kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, Lupa atazikwa Jumapili, Juni 9, 2024.
Marehemu Milton Lupa alikuwa na Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kupata diploma ya uzamili ya uhasibu kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM).
Pia alikuwa na shahada ya kwanza ya biashara na usimamizi (B.comm) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, CPA (T) chini ya kundi la Associate na pia alikuwa na diploma ya Usimamizi wa Mifumo ya Afya ambayo aliipata kutoka Chuo cha Galillee nchini Israel.