Marehemu Nyaulawa, kuugua mpaka kufa kwake

RIP Mh Nyaulawa.

Inv. alikuwa anasumbuliwa na kansa ya utumbo aliwahi kulazwa Apollo Hosp India kwa muda mwaka huu.



Nashukuru mkuu Masatu kwa kunifahamisha juu ya hili.

 
Mungu amrehemu, mchango wake utaendelea kukumbukwa
 

Inamaanisha A-level Education hakusoma?
Akarukia kwenye Bussiness College Diploma in Bussiness.
Naomba ofafanuzi hapo.
 



Nashukuru mkuu Masatu kwa kunifahamisha juu ya hili.

Inv Twashukuru kwa info na naomba niungane na wafiwa wote kumtakia marehemu huyu alale kwa amani, out of that pia naomba kuwahimiza wapiga kura wa hilo jimbo kuwa SASA NI WAKATI WA KULETA MABADILIKO NCHINI KWETU SO NI VYEMA TUKAPIGIA KURA CHAMA PINZANI ILI KUONGEZA CHALLENGES KWA SERIKALI YETU PALE BUNGENI.

YES WE CAN
 
RIP Mheshimiwa Nyaulawa, hiyo ndio njia ambayo nasi tutaipitia. Siku na saa ndio hatuijui.
 
"Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe"
Poleni wafiwa, amani yake Mungu wetu iwafunike katika kipindi kigumu hiki.
 
Pole afiwa maana sasa kafikisha mwisho wake. Tutakutana huko Mbinguni
 
Inamaanisha A-level Education hakusoma?
Akarukia kwenye Bussiness College Diploma in Bussiness.
Naomba ofafanuzi hapo.

Kuna cha ajabu hapa. Ni ni lazima uende A level ndo upate degree? lol
RIP Richard Nyaulawa
 
May His Soul Rest In Peace Amen!
 
Inamaanisha A-level Education hakusoma?
Akarukia kwenye Bussiness College Diploma in Bussiness.
Naomba ofafanuzi hapo.

Halafu ukishaupata ndio iweje? ligi nyingine hizi...
 
RIP Richard Nyaulawa! Mkoa wa mbeya tumepoteza mtetezi wetu na mpiganaji hodari.

Ukimaliza Form IV unaqualify kusoma Diploma kwa hapa nchini na ukifaulu vizuri unaweza kusoma Degree ya kwanza.Ikumbukwe kwamba Diploma ya CBE inasomwa kwa miaka miwili hivyo kufananishwa kwa kiasi fulani na aliyesoma A-Level.

Nafikiri mkuu Fidel80 tuko pamoja!
 
..kuna siku nilipost hapa kuwa alikuwa mgonjwa sana ...siku hiyo ndio alikuwa amerudishwa kutoka india baada ya juhudi za kumtibu kansa ziliposhindikana....MUNGU AMREHEMU.......!!!

NDUGU WANA JF ..UNAPOONGELEA WATANZANIA WAJASIRIAMALI AGGRESSIVE..WAZAWA..JINA LA RICHARD NYAULAWA ...LITACHOMOZA....
NI MTU ALIYEKUWA HAPENDI KUJIONESHA ..NADHANI ANGEPENDA KUJULIKANA ..ANGEJULIKAANA ZAMANI...SANA..KWANI HUYU AMEANZA KUMILIKI GAZETI KABLA YA MENGI...MOJA YA MAGAZETI YA KWANZA ..MAJIRA NA BUSINESS TIMES....KUNA WAKATI YALIKUWA TOP SELLING.......LAKINI WAANDISHI WAKE AMBAO NA HUMU WAMO...HAWAKUWA NA INSTRUCTIONS ZA KUMTANGAZA TANGAZA.....

ANAMILIKI MAKAMPUNI MENGINE..PIA KWA KUSHIRIKIANA NA WAZAWA WENGINE KAMA MZEE MBUGUNI..na wengine,hawa na wenzao wengine walikuja kuanzisha BENKI YA KWANZA KUMILIKIWA NA WAZAWA........FIRST ADILI BANK...BAADAYE WALIFANIKIWA KUWAUZIA SHARE NSSF..NA BENKI SAA INAITWA ....AZANIA BANKCORP..........

MUHESHIMIWA RICHARD NYAULAWA R.I.P...TUNAWEZA KUMPA HESHIMA LAKINI INAWEZA IKAWA HAITOSHI...KUTOKANA NA TABIA YAKE YA KUWA LOW PROFILE..NINA IMANI KUBWA KUWA MUNGU ATAMNYANYUA KWA NIABA YETU....KAMA MWENYEWE ALIVYOAGIZA KWENYE MAANDIKO..KUWA ATAWAINUA WASIOJIKWEZA!!!!
 

Poleni sana familia na wana Mbeya Vijijini. Hakushiriki pia kuanzisha ACB?+Bussiness Care nk? Nani kumrithi kupitia CCM yetu? Najua pale CHADEMA hawana chao, sio kama Tarime

.....ndiyohiyo
 
Ukimaliza Form IV unaqualify kusoma Diploma kwa hapa nchini na ukifaulu vizuri unaweza kusoma Degree ya kwanza.Ikumbukwe kwamba Diploma ya CBE inasomwa kwa miaka miwili hivyo kufananishwa kwa kiasi fulani na aliyesoma A-Level.
Asanteni kwa ufafanuzi.
RIP Richard Nyaulawa, tunazidi kumuomba Mola ailaze roho ya marehemu pema peponi, Amina.
 
Poleni sana familia na wana Mbeya Vijijini. Hakushiriki pia kuanzisha ACB?+Bussiness Care nk? Nani kumrithi kupitia CCM yetu? Najua pale CHADEMA hawana chao, sio kama Tarime

.....ndiyohiyo

..AKIBA PIA ni ya wazawa lakini ni ya pili kuanzishwa baada ya FIRST ADILI....Nafikiri wazawa wenye interest kwenye ACB ni kina IDRISSA RASHID....aliisaidia sana hii benki ya akiba kijipanua kwenye wigo wa SME"S.....alianzisha sera ya mabenki kuwalenga watu wa chini kabla hata ya NMB na wengine kufuata..tatizo ACB hawakuwa na mtaji mkubwa sana....lakini inaheshimika..na misingi ya benki hiyo leo imewekwa na IDRISSA RASHID.....
 
Kuna cha ajabu hapa. Ni ni lazima uende A level ndo upate degree? lol
RIP Richard Nyaulawa
haisaidii kujua kama alipita A level au laa hapa la msingi mwenzetu ametangulia mbele ya haki mungu ailaze mahali pema peponi.Aidha mungu aifariji familia yake kwa wote ni njia yetu amen
 
poleni sana wananchi na familia ya marehemu nyaulawa, by the way wabunge wa mbeya vijijini kuna nini? hombee, yete malyego na sasa nyaulawa wanakufa kabla ya kumaliza kipindi chao cha ubunge! anyway GO SO GREAT
 
rip mh. nyaulawa. namuomba mola awafariji ndugu na jamaa
wa marehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…