Kwa wale watakopenda kushiriki katika safari ya mwisho ya kumsindikiza Mbunge wetu,
Mwili wa Marehemu utawasili nyumbani kwake Mtaa wa Mzimuni, Kawe Majumba Sita, Barabara mpya ya kuelekea Bahari Beach siku ya Jumatano Saa Nne Kamili Asubuhi, na Kufuatiwa na Ibada ya Kuuaga Mwili wa Marehemu na Buriani Katika Kanisa Katoliki alilokuwa anasali la Mtakatifu Martha - Mikocheni (Kwa warioba). Ibada kanisani hapo itaanza saa Saba Mchana. Kwa yeyote yule na kwa imani zetu tofauti, tuungane kumuombea apumzike kwa Amani......
Raha ya Milele Ampe ee Bwana, Na Mwanga wa Milele Amuangazie,
Marehemu Apumzike kwa Amani. Amina.