Marehemu

Edmund

Senior Member
Joined
Jul 17, 2009
Posts
123
Reaction score
62
Baba yangu alifariki mwaka jana mwezi wa saba, katika harakati za kufuatilia mali zake tukakuta kumbe nyumba moja imeshauzwa kwa Mpangaji anaekaa humo ndani kitambo tu. baada ya kupekua nyaraka za marehemu hatukukuta hata chembe ya "document" kuonyesha kuwa imeuzwa, Lakini katika zile hati za mauzo kati ya Marehemu yaani BABA na Mnunuzi yaani yule (Mpangaji). kuna mashahidi wa3 yaani Mununuzi, Mkewe na mtoto wao, kwa upande wa muuzaji alikuwepo pekee yake pamoja na Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa eneo husika

JE, ni kweli haya yatakuwa mauzo halali kisheria.
 
pole sana,huwezi jua kwa nini baba yako aliiuza hio nyumba kisirisiri-financially baba akistrugle atahangaika mwenyewe kutafuta ufumbuzi,hio ni kawaida ya wanaume kutoshirikisha familia sometimes kny mambo kama hayo,ingawa sina uhakika kama kweli aliuza au la.....ungeiweka kule jukwaa la sheria labda ungepatiwa muongozo,huku MMU tunataniana sana sidhani kama utapatiwa msaada unaohitaji.
 
mama hawezi kuwa shahidi wa baba kisheria. Wanatambulika kawa ni mwili mmoja mbele ya jicho la sheria.
 
Tafuta ushauri wa kisheria.....:coffee:
 

Haya ni Manunuzi halali kabisa iwapo marehemu baba yako alikuwa na akili timamu....na hakushinikizwa na mtu kufanya hivyo... hasa ikionekana kuwa yeye mwenyewe amesaini. Nashauri uchunguze kama ni kweli alisaini na kama saini ni yake kweli basi itakuwa ngumu kukomboa... Pia mjumbe wa serikali ya mtaa akitoa ushuhuda uwepo wake waweza kuwa na nguvu kama ule wa wakili... Poleni sana lakini endelea kupigana waweza kupata tundu la kukomboa mali yenu
 
nijuavyo mimi, kuna consent ya spouse kwenye hayo mambo (kama ni mke wa halali) na sheria za mirathi zinaweza kumtetea mjane au watoto

wapo humu akina buchanan wa-PM uone raha
 
Edmund,

Habari yako, natumaini uko salama. Nimeshtuka sana nilipoona hii thread kwenye email yangu. Sikuwahi kuisoma wala ku-comment. Nimeshangazwa na mtu aliyejibu 'sasa'. Nashindwa kuelewa nini kimetokea lakini kuna uwezekano mkubwa mtu akawa ametumia jina langu vibaya ikiwa ni pamoja na kulog in kwa kutumia jina langu.

Hili si suala la jumuiya hivyo ningependa kukushauri in private ya nini cha kufanya na endapo utafanikiwa unaweza kurudi kuwajulisha wanaJF.

Vinginevyo nakutia moyo kwamba kama haki ni yako haitapotea ukiipigania.

My contacts are public, 0767 533 433. just drop me a text.

albert.
 
Je signature ya Mzee wako?
 


Wizi huo Mkuu! Fuatilia udai haki yenu...
 
ushauri wangu: ipeleke jukwaa la sheria unaweza pata msaada mkubwa zaidi kwani limekaa kisheria zaidi. Kumbuka kuna wanasheria wazuri tu humu JF lakini hawapitii jukwaa hili kabisa.
 
ushauri wangu: ipeleke jukwaa la sheria unaweza pata msaada mkubwa zaidi kwani limekaa kisheria zaidi. Kumbuka kuna wanasheria wazuri tu humu JF lakini hawapitii jukwaa hili la MMU kabisa.
 
Marehemu alipaswa kupata CONSENT ya mama yenu kama yupo.Je alifanya hivyo? Kama hakuna basi mauzo ya nyumba ya familia ni batili kisheria.

Haraka nenda Idara ya usajili wa hati ukaone kama kuna kitu kama hicho maana wakati mwingine kunakuwepo na ama hati za kughushi au hati halali ambayo huenda mama aliweka sahihi kukubali kitu asichokijua.

Tafuta wakili akusaidie ( Albert Msendo keshakupa contacts hapo juu) au kama huna uwezo tafuteni msaada wa kisheria
 
Mada ipeleke jukwaa la sheria. Kule kuna wanasheria waliobobea. Utapata ushauri mzuuuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…