Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Inaonekana marejesho ya mikopo bubu ya mali kauli, ile mikopo ya kijumbe, ile michezo ya kutuzana fedha kwa zamu kwa mzunguko wa wiki au mwezi na mikopo ya vikoba imechochea na kuchangia kwa kiasi fulani ongezeko la wizi na udokozi wa vitu mbalimbali humu nchini.
Hayo yote yanafanyika ili kumeet deadline ya siku ya marejesho ya mikopo na kuepuka ongezeko la deni, faini ya kuchelewesha marejesho ya mkopo, na kupoteza uaminifu wa kukopeshwa tena mbeleni..
Licha ya kwamba kadhia hii ya wizi na udokozi wa aina mbalimbali imewakumba watu wengi sana maeneo tofauti tofauti mijini na vijijini, songombingo hiyo imenikumba pia mimi kiongozi mwaninifu na mchapakazi wa wananchi, katika mashamba kadhaa miongoni mwa mashamba yangu ya mazao ya biashara, ambayo pia ni sehemu ya kitega uchumi changu cha maana sana, kinachonipatia fedha nyingi sana za kujikimu, kuendesha familia na kuboost miradi yangu mingine kama vile ufugaji.
Baada ya kufanya utafiti wa kina juu ya wizi na uporaji huo mbaya katika mashamba yangu, nilibaini na kujiridhisha pasina shaka kwamba, wizi ule haukufanyika kwasababu ya njaa, bali wezi wamelazimika kufanya hivyo, ili kuwahisha marejesho ya mikopo waliokopa hususani kwa wapopeshaji binafsi wa kali sana pale kijijini, na ili kuepuka kuporwa mali zao nyingine kwenye familia zao, kama vile kuku wakubwa walionona au mbuzi wa gharama kubwa ukilinganisha na kiwango kidogo sana cha mkopo wenyewe waliokopa..
Kwa mfano, katika moja ya mashamba yangu ya mazao ya kibiashara, wezi wameiba kwa kuvuna mbaazi zilizokua zimesitawi, zimekomaa na kukauka vizuri sana kwa zaidi ya ekari4, kati ya ekari20 nilizolima zao hilo muhimu sana, la thamani na ghali mno la mbaazi.
Nimesikitika sana, nimefadhaika sana lakini namshukuru Mungu sana kwa kile ambacho nimefanikiwa kukivuna kwa mwaka huu mzuri na muhimu sana kwa kilimo.
Kama kiongozi, nitaendelea kutoa elimu kwa wananchi, na kwamba suluhisho la kua na uhakika wa kipato na kurejesha mikopo tunayokopa ni kua na nidhamu ya matumizi ya fedha hizo za mkopo, bidii na kuzitumia fedha hizo kwa usahili na umakini mkubwa, kufanikisha malengo mahususi, hususani ya uzalishaji, na kwamba wizi ni anasa inayoweza kuhatarisha haiba, afya na hata maisha yako.
Acha wizi, fanya kazi kwa bidii 🐒
Mungu Ibariki Tanzania