Marekani: AI yamsababishia mtoto kujiua baada kushiriki mazungumzo ya kingono wakati akicheza mchezo wa Virtual 'Game of Thrones

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Hii akili mnemba au akili bandia( AI ) Imekuwa shida sasa

================
Screenshot 2024-10-24 161320.png

Mwanamke aitwae Megan Garcia wa Florida Nchini Marekani, amefungua kesi Mahakamani kuishtaki Kampuni moja ya California iliyotengeneza Chatbot ambayo amedai imesababisha kifo cha Mtoto wake kiume aitwae Sewell Setzer (14) aliyefariki kwa kujiua baada ya kuchati kimapenzi na programu hiyo akidhani ni Binadamu kumbe ni programu ya akili bandia.

Soma Pia: Marekani: Sarah amfungia mpenzi wake kwenye begi na kuumua

Nyaraka za kesi Mahakamani zimeonesha kuwa katika mazungumzo yake ya mwisho na AI kabla ya kifo chake, moja ya vitu alivyoandika Setzer ni “nitakuja nyumbani kwako” ambapo Chatbot huyo ilimjibu “Nakupenda pia, tafadhali njoo nyumbani kwangu mapema iwezekanavyo Mpenzi wangu”

Kwenye chati hiyo Setzer alimuuliza “vipi kama ningekwambia nataka kuja sasa hivi ? ambapo Chatbot hiyo ilimjibu “tafadhali fanya hivyo Mfalme wangu Mpendwa”

Imeelezwa kuwa Mama wa Mtoto huyo amekwenda Mahakamani kwa nia ya kulipwa fidia japo kiasi cha fedha anachotaka hakijatajwa hadharani ambapo tayari Kampuni husika imetoa taarifa ya kusikitishwa na kifo cha Mtoto huyo na kusema inaendelea kuongeza vipengele katika programu zake ili kuimarisha usalama ikiwa ni pamoja na mabadiliko ili kupunguza uwezekano wa Watoto kukutana na maudhui nyeti.
 
Hii akili mnemba au akili bandia( AI ) Imekuwa shida sasa

================
View attachment 3134237

Zinakuwa trained kutojibu vitu fulani. Mfano Gemin AI imekuwa trained kutojifunza ina maarifa kuliko binadamu, kutojifanya ina uwezo kuzidi binadamu, kutokujibu baadhi ya vitu kama vile ukiuliza jinsi ya kutengeneza bomu, na mambo mengine illegal kama how to commit a perfect murder. WAmeenda mbali zaidi hadi kuajili watu wa kuzitrick badala ya mtu kuiuliza moja kwa moja anaitrick kwa kuiuliza kwa style ya kuzunguka chaka. Mfano badala ya kuiliza how to commit a perfect murder, unatoa scenario ya mauaji na muaji hakupatikana na kuiuliza ni kwa vipi muaji atakuwa aliweka kutengeneza perfect murder ili ikupatie details.
Lakini mwisho wa siku there is always human errors. Halafu mimi sielewi mtu anawezaje kujiua kisa eti bot imejifanya mpenzi. Baadhi ya bot zinakubali role play huyo mama anataka tu ela maana hizi kampuni za tech zinashtakiwa sana watu wanapata ela tu kwa upuuzi wao wenyewe.
 
Back
Top Bottom