Mheshimiwa Rais Joseph Biden wa Marekani amemteua Bibi Kilolo Kijakazi kuwa Kaimu Kamishna wa Shirika la Hifadhi ya Jamii, Social Security Administration.
Uteuzi wa Mama Kijakazi unafuatia kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Bwana Andrew Saul ambae alikataa kujiuzulu mwenyewe alipoombwa afanye hivyo na Rais Biden.
Bwana Saul, ambae aliteuliwa na Rais wa awamu ya 45, Bwana Donald Trump, amepinga vikali kutumbuliwa kwake akidai Rais hana mamlaka ya kumfukuza kazi kwa vile uteuzi wake unalindwa kikatiba , jambo ambalo limepingwa na Rais Biden akirejea uamuzi wa nyuma wa mahakama ya rufaa ya nchi hiyo ambao Rais amedai unampa mamlaka hayo.
Bwana Saul amesema ataripoti kazini kama kawaida Jumatatu asubuhi kwa kujiunga kwenye mtandao wa shirika akiwa nyumbani kwake na kuchapa kazi.
Mama Kilolo Kijakazi ndie aliyewafahamisha wafanyakazi wenzie kwa njia ya barua pepe kwamba ameteuliwa kukaimu uongozi wa taasisi hiyo huku akimshukuru Bwana Saul kwa utumishi wake wa umma.