Marekani: Amuua Jirani yake ambaye alidai kuwa ni Shetani

Marekani: Amuua Jirani yake ambaye alidai kuwa ni Shetani

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wakuu Salama!

Nimeshangazwa na hii taarifa yani mshikaji kampiga kisu mwezie kisa alidhani ni shetani. Mhhh hii sasa inatisha sana.
====================

Mwanamume mmoja wa New Orleans Nchini Marekani aitwae Jerry Gelpi aliyedai kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumchoma kisu na kumuua Jirani yake aitwae Charles Davis (68) ambaye alidai kuwa ni Shetani/Pepo.

Waendesha mashtaka wamesema kuwa Jerry aliingia katika nyumba ya Jirani yake huyo February 2021 na kumchoma kisu mara 16 hadi kufa akiwa bafuni na kisha akatoroka eneo la tukio ambapo wakati wa kesi, Gelpi alidai kuwa yeye ni Mwana wa Mungu na kwamba Davis alikuwa Pepo mwenye nguvu zaidi.

Soma Pia: Atupwa jela kwa kosa la kumchoma kisu jirani hadi kumuua kisa kukoroma


Awali Gelpi alikana kuhusika na mauaji hayo lakini uchunguzi zaidi ulifichua makosa mengine mawili kwenye video za CCTV na vipimo vya DNA, hatia ambayo imemfanya ahukumiwe kifungo cha maisha jela bila msamaha.
 
Back
Top Bottom