Marekani inatakiwa kuwajibika kwa vitendo kupunguza utoaji wa gesi chafu

Marekani inatakiwa kuwajibika kwa vitendo kupunguza utoaji wa gesi chafu

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1.jpg


Upunguzaji wa utoaji wa gesi chafu hauwezi kufanikiwa bila ya kuwa na vitendo halisi kutoka kwa nchi zilizoendelea. Katika kipindi cha Utawala wa rais Donald Trump, Marekani iliojiondoa kwenye mkataba wa Paris na kuonyesha kuonyesha dunia mtazamo usiofaa kwenye juhudi za kulinda mazingira.

Hata hivyo baada ya Marekani kurejea kwenye mkataba huo chini ra rais Joe Biden, China imeendeleza wito kwa Marekani kupunguza utoaji wa gesi chafu. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin hivi karubuni amesema Marekani inapaswa kupunguza utoaji wa gesi chafuzi wakati ripoti zikibaini ongezeko utoaji wa gesi hiyo la asilimia 6.2 nchini Marekani mwaka 2021.

Bw. Wang alisema hayo akijibu hoja kuhusu kuongezeka kwa asilimia 17 ya uzalishaji wa nishati ya makaa ya mawe mwaka 2021. Uzalishaji huo umetajwa kuwa chanzo kikuu cha kupaisha uchafuzi wa mazingira nchini Marekani na ambao sasa umefanya kuongeza muda wa malengo ya kukabiliana na hali ya hewa yake ya mwaka 2025 na 2030. Bw. Wang aliitaka Marekani kuchukua hatua ya kupunguza hewa chafu badala ya kuwa "Mrusha Tiara."

Bw. Wang anasema kama nchi iliyoendelea na mtoaji mkuu wa gesi chafu, Marekani inapaswa kuacha kuzilaumu nchi nyingine na kuanza kuzingatia mambo yake ya ndani na wakati huo huo kujiepusha na maneno bila vitendo.

"Kuongezeka kwa uzalishaji wa gesi chafu nchini Marekani kunatukumbusha tena kwamba tunapoweka shabaha za kupunguza hewa chafu, tunapaswa kuwa na malengo na busara, kuzingatia kanuni ya uwajibikaji wa kawaida lakini tofauti, na kuzingatia hali tofauti za kitaifa. Hatupaswi kulenga juu sana au kuinua malengo kwa nia ili kujipatia umaarufu au kuzuia haki halali za maendeleo na maslahi ya nchi zinazoendelea," Anasema Bw. Wang.

Katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, China siku zote imekuwa nchi ya utekelezaji, inayobeba kikamilifu majukumu ya kimataifa yanayolingana na hali yake ya kitaifa na kuongeza jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Tangu Septemba 2020, baada ya kutimiza zaidi malengo ya hatua ya kukabliana na mabadiliko ya tabia nchi mwaka 2020 kabla ya ratiba, China ilitangaza lengo na maono ya kilele cha kaboni na kutoegemea gesi hiyo chafu. China pia iliweka malengo mapya ya Michango Iliyodhamiriwa ya Kitaifa na kutangaza mfumo wa sera ya "1+N" wa kutokuwa na kaboni.

Takwimu

Wanasayansi wanapopima utoaji wa hewa chafu, wanachunguza jumla ya uzalishaji ambao nchi inatoa hewani kwenye ardhi yao wenyewe kila mwaka. Uzalishaji huo hutoka kwa kitu chochote kinachoendeshwa na nishati ya kisukuku, kama vile kuendesha magari yanayotumia petroli, usafiri wa anga , kupasha joto na taa kwa nishati inayotokana na makaa ya mawe, gesi asilia au mafuta. Vyanzo vingine, kama vile uzalishaji kwa ukataji miti.

Ikilinganishawa na Marekani, nchi hiyo inawajibika kwa utoaji wa uchafu wa tani bilioni 5.7 ambayo ni asilimia11% ya jumla ya uzalishaji wa gesi chafu, ikifuatiwa na India 6.6% na Umoja wa Ulaya 6.4% . Na kwa jumla, Marekani imetoa karibu mara mbili ya kaboni ikilinganishwa na China tangu 1850.
 
Back
Top Bottom