#COVID19 Marekani inatarajia kutoa 'booster vaccine' kwa watu wote waliopata chanjo

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Leo Jumatano, serikali ya Marekani inatarajia kutangaza kuanza kutoa chanjo ya pili kwa wale waliopata chanjo ya J&J ama ya tatu kwa waliopata chanjo zingine za kukabiliana na covid 19 kwa watu wote waliopata chanjo.

Awali, wiki iliyopita, taasisi ya afya na chakula ya Marekani, FDA ilitoa kibali kwa booster vaccine kwa wale wenye umri wa miaka 60 ama zaidi ama wale wenye magonjwa na ambao kinga yao ya mwili imeshuka, kitaalam wanaitwa immunocompromised patients.

Hii imetokana na ushahidi kutoka Marekani na Israel umeonyesha kua chanjo hupoteza uwezo wake ama ufanisi baada ya miezi 6 toka mtu amechanjwa hivyo anahitaji chanjo nyingine ili kuendelea kumpa mtu kinga zaidi.

Israel wao wameanza kutoa chanjo ya booster kwa watu wote. Hii pia ni baada ya kushuhudia kuongezeka kwa wagonjwa na vifo kwa watu waliochanjwa chanzo zote. Israel ni taifa ambalo limefanikiwa sana kwenye chanjo ya awali baada ya kuchanja zaidi ya 70% ya watu wake.

Ngwajima theory proof , chanjo imedunda , inahitaji msaada (Booster)
Nilichogundua Tanzania tunasafari ndefu sana yakufikia nchi ya ahadi....!!!'' hatuna utulivu kwenye masuala muhimu kama haya ya afya za watu wa nchi yetu!!! Kama hii habari niya kweli basi viongozi wanapaswa kuwajibika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichogundua Tanzania tunasafari ndefu sana yakufukia nchi ya ahadi....!!!'' hatuna utulivu kwenye masuala muhimu kama haya ya afya za watu wa nchi yetu!!! Kama hii habari niya kweli basi viongozi wanapaswa kuwajibika

Sent using Jamii Forums mobile app
Tabu kubwa , hii habari hata kama siyo kweli inaleta hofu kwa waliochanjwa.
 
Ngwajima theory proof , chanjo imedunda , inahitaji msaada (Booster)
They just want total protection

death due to Covid Kwa alaiochanjwa ni negligible compared to unvaccinated
 
Leo Jumatano, serikali ya Marekani inatarajia kutangaza kuanza kutoa chanjo ya pili kwa wale waliopata chanjo ya J&J ama ya tatu kwa waliopata chanjo zingine za kukabiliana na covid 19 kwa watu wote waliopata chanjo.

Awali, wiki iliyopita, taasisi ya afya na chakula ya Marekani, FDA ilitoa kibali kwa booster vaccine kwa wale wenye umri wa miaka 60 ama zaidi ama wale wenye magonjwa na ambao kinga yao ya mwili imeshuka, kitaalam wanaitwa immunocompromised patients.

Hii imetokana na ushahidi kutoka Marekani na Israel umeonyesha kua chanjo hupoteza uwezo wake ama ufanisi baada ya miezi 6 toka mtu amechanjwa hivyo anahitaji chanjo nyingine ili kuendelea kumpa mtu kinga zaidi.

Israel wao wameanza kutoa chanjo ya booster kwa watu wote. Hii pia ni baada ya kushuhudia kuongezeka kwa wagonjwa na vifo kwa watu waliochanjwa chanzo zote. Israel ni taifa ambalo limefanikiwa sana kwenye chanjo ya awali baada ya kuchanja zaidi ya 70% ya watu wake.

Mkuu ni kweri kabisa maana hata mm niliangalia utv jana saa 4 uck walisema.
 
Hii imetokana na ushahidi kutoka Marekani na Israel umeonyesha kua chanjo hupoteza uwezo wake ama ufanisi baada ya miezi 6 toka mtu amechanjwa hivyo anahitaji chanjo nyingine ili kuendelea kumpa mtu kinga zaidi.
Kwanza heading yako ipo too exaggerated!! Kuhusu suala la miezi 6, hilo linafahamika.
 
They just want total protection

death due to Covid Kwa alaiochanjwa ni negligible compared to unvaccinated
Ni kweli, ila sasa hiki kirusi kinatabia ya kubadilika badilika, kwahiyo kila baada ya miezi 6 mtu ukaachanjwe booster, this is impractical, tule matunda na tufanye mazoezi huku tukiruhusu mwili kutengeneza natural immunity. Labda kwa wale highly compromised, ila sio msema kila mtu akachanjwe, ni illogical.
 
Back
Top Bottom